Kibukusu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyumba ya jadi ya wazungumzaji wa Kibukusu.

Kibukusu (jina la asili: Lubukusu) ni lugha ya Kibantu nchini Kenya inayozungumzwa na Wabukusu. Ni moja kati ya lugha zinazohusiana na Waluhya. Pia, inahusiana na lugha za Gisu na Masaaba za Uganda Mashariki: lugha hizo zote zinaweza kuelewana.

Mwaka wa 2009 idadi ya wasemaji wa Kibukusu ilihesabiwa kuwa watu 1,433,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kibukusu kiko katika kundi la E.30, hasa moja ya lugha za Kiluhya.

Lahaja[hariri | hariri chanzo]

Lugha hii ina lahaja tatu muhimu:

Kati ya hizi, lugha inayozungumzwa karibu na Kitale inachukuliwa kuwa ya asili zaidi. Hii ni kwa kuwa lahaja hizo nyingine mbili zimeingiliwa na ushawishi wa lahaja nyingine za lugha za Kiluhya.

Ushawishi wa lugha nyingine[hariri | hariri chanzo]

Wabukusu wanaishi katika Wilaya ya Bungoma ambayo inapakana na Uganda kuelekea Magharibi na Wilaya ya Kakamega ya Kenya kuelekea Mashariki.

Katika mpaka wa Uganda, wanaishi BaMasaaba na BaGisu, ambao wanahusiana na Bukusu kupitia lugha moja na utamaduni unaofanana.

Kuoana kati ya Bukusu na jamii hizo ni jambo linaloungwa mkono na jamii zote. Matokeo ni kuwa Wabukusu wana jamaa wa karibu katika jamii hizi, na jamii hizi pia zina jamaa kati ya Wabukusu.

Wakati wa Vita vya Uganda miaka ya 1970, wengi wa BaGisu na BaMasaaba walitoroka Uganda na kuhamia Kenya ili kuishi na jamaa zao wa Bukusu karibu na Bungoma. Vita vilipokwisha wengi wao hawakurudi Uganda.

Kuenea kwao kati ya Bukusu kumekuwa na ushawishi mkubwa kwa lugha ya Bukusu katika maeneo ya Bungoma. Wazungumzaji wa asili wa Bukusu wanaweza kutambua mtu kutoka eneo la Bungoma kutokana na lugha yake. Kwa mfano wanatumia L badala ya R, na hivyo kitenzi 'khuufwara'- kuvaa nguo sasa linatamkwa 'khufwaala' jinsi linavyotamkwa na BaGisu na BaMasaaba.

Lahaja inayotumiwa mashariki mwa mji wa Webuye ina ushawishi wa lahaja jirani, Kabras na Tachoni za lugha za Kiluhya. Hili linaonekana katika kubadilisha mwanzo wa nomino. Kwa mfano, nomino 'sisindu' (kitu fulani) inatamkwa 'eshindu' katika Kabras. Wabukusu wa Webuye huiita 'esindu'.

Kwa vile wanapakana na Waniloti na lugha za Kikalenjin za Pokot, Nandi na Sebei kuelekea kaskazini, mashariki na magharibi, lugha ya Bukusu ya Kitale imehifadhi kwa ukubwa uasili wake. Ni tofauti kabisa na lahaja nyingine zilizozungumziwa awali.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • De Blois, Kornelis Frans (1975) 'Bukusu generative phonology and aspects of Bantu structure' (Annales de MRAC, no. 85). Tervuren: Musщe Royal de l'Afrique Centrale.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]