Nenda kwa yaliyomo

Enzi ya kati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Karne za Kati)
Kanisa la Mt. Mikaeli mjini Hildesheim (Ujerumani) ni mfano bora wa usanifu majengo wa Enzi ya kati.

Enzi ya Kati (pia: Zama za Kati; kwa Kiingereza: "Middle Ages", pia "mediaevo" au "medievo") ni kipindi cha katikati cha historia ya Ulaya katika mgawanyo wa “zama” tatu: ustaarabu wa

ama:

Hata kama ugawaji huo umetokana na mazingira ya Ulaya tu, hutumiwa pia kwa maeneo mengine ya dunia. Wataalamu wengi huamini ya kwamba haufai sana kidunia lakini hadi sasa hakuna mpangilio mwingine kwa dunia yote unaoeleweka kirahisi hivi.

Kwa kawaida, Zama za Kati za Ulaya Magharibi huhesabiwa toka mwisho wa Dola la Roma Magharibi (karne ya 5) hadi kuanza kwa falme za kitaifa, mwanzo wa uvumbuzi wa ng’ambo ya Ulaya, kipindi cha mwamko-sanaa, na Matengenezo ya Waprotestanti kuanzia mwaka 1517.

Mabadiliko hayo yalionesha mwanzo wa kipindi cha Zama za Kisasa ambacho kilitangulia mapinduzi ya viwanda.

Mwanzo wa kipindi cha Enzi ya Kati

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya Enzi ya Kati kulikuwa na ustaarabu wa Dola la Roma. Milki hiyo kubwa ilijenga utamaduni uliounganisha nchi za Afrika ya Kaskazini, Asia ya Magharibi na Ulaya ya Kusini pamoja na Ulaya ya Magharibi.

Katika eneo hili kubwa palikuwa na uchumi ulioendelea na njia za mawasiliano kama barabara, bandari na hata aina ya posta.

Ustaarabu huo ulikuwa na idadi ya watu waliojua kusoma na kuandika. Lugha za pamoja kama Kilatini na Kigiriki zilieleweka na asilimia fulani ya watu kote katika dola hili. Hata kama watu wengi, hasa watu wa vijijini na watumwa, hawakujua kusoma bado walikuwepo watu waliojua kila sehemu ya dola.

Ustaarabu huo uliporomoka pamoja na matatizo ya kiuchumi, gharama kubwa ya jeshi, kupungua kwa uzazi na mashambulio ya makabila ya nje, hasa ya Wagermanik, yaliyoweza kuingia ndani ya Dola la Roma bila kulingana na utamaduni wa ustaarabu huo. Roma ilishindwa kutunza utaratibu wake mbele ya mashambulio na uhamisho mkuu wa Ulaya.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Enzi ya kati kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.