Nenda kwa yaliyomo

Tambarare ya Uhindi Kaskazini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Indo-Gangetic Plain)
Maeneo ya tambarare ya Uhindi Kaskazini.
Mashariki mwa tambarare (India, Bangladesh na Nepal) kwa macho ya satelaiti; Mto Ganges uko katikati ya tambarare.

Tambarare ya Uhindi Kaskazini ni eneo kubwa la bara upande wa kusini wa Milima ya Himalaya linaloshika Uhindi Kaskazini yote na Bangladesh yote pamoja na sehemu za Pakistan na Nepal.

Tambarare hiyo imesababishwa na mito miwili ya Indus na Ganges na ina kilomita za mraba milioni 2.5[1]. Inakaliwa na watu bilioni 1 yaani sehemu ya saba ya watu wote duniani.

Tambarare yote imegawiwa katika mabeseni ya mito miwili: maji upande wa magharibi huelekea mto Indus na upande wa mashariki huelekea mto Ganges.

Tambarare hiyo inapokea maji yake kutoka milima ya Himalaya hasa; mito hiyo imetelemka pamoja na matope yaliyojenga tabaka nene la ardhi yenye rutuba. Hivyo ni eneo linalofaa kwa kilimo hasa cha mpunga na ngano kinacholisha idadi kubwa ya watu.

Katika historia ya binadamu ilikuwa kati ya maeneo ya kwanza ambako milki na utamaduni wa miji vilianzishwa vikiwezesha kuwepo kwa wataalamu walioweka misingi ya sanaa na elimu ya juu.[2]

  1. Taneja, Garima; Pal, Barun Deb; Joshi, Pramod Kumar; Aggarwal, Pramod K.; Tyagi, N. K. (2014). Farmers preferences for climate-smart agriculture: An assessment in the Indo-Gangetic Plain. Intl Food Policy Res Inst. uk. 2.
  2. "India". CIA – The World Factbook. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Juni 2008. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2007. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tambarare ya Uhindi Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.