Nenda kwa yaliyomo

Hifadhi ya Banc d'Arguin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Banc d'Arguin

Hifadhi ya Banc d'Arguin (kwa Kiarabu: ) kwenye Hori ya Arguin iko kwenye pwani ya Mauritania kati ya Nouakchott na Nouadhibou kwenye eneo la kilomita za mraba 12,000. Jina linatokana na Kisiwa cha Arguin kilichopo karibu na pwani hiyo.

Hifadhi hiyo imeandikishwa katika orodha ya Urithi wa Dunia ikiwa ni eneo muhimu la kuzaliana kwa ndege wahamiaji kutoka Afrika na Ulaya. Bahari mbele ya pwani hiyo ni kati ya sehemu zenye samaki wengi katika Afrika ya Magharibi pamoja na kuwa sehemu muhimu kwa kuzaa kwa samaki.

Hifadhi ya Kitaifa ya Banc d'Arguin ni hifadhi ya mazingira ambayo ilianzishwa mnamo 1976 kulinda rasilimali zote za asili na uvuvi, ambao hutoa mchango mkubwa kwa uchumi wa taifa. Hifadhi inatembelewa kila mwaka na zaidi ya milioni mbili ndege wahamiaji kutoka Ulaya ya Kaskazini, Siberia na Greenland.

Maboti ya uvuvi huko Banc d'Arguin.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya wakazi si zaidi ya watu 500 wa kabila la Imraguen ambao wanaishi katika vijiji saba ndani ya hifadhi. Wana uchumi wa uvuvi wa kujikimu kwa kutumia njia za jadi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Eneo la hifadhi ya leo liligombaniwa na mataifa mbalimbali ya Ulaya na Afrika ya Kaskazini kwa karne nyingi.

1445   - 5 Februari 1633 Utawala wa Ureno (Arguim).
5 Februari 1633   - 1678 Utawala wa Uholanzi (kipindi kifupi chini ya Uingereza mnamo 1665).
1 Septemba 1678   - Septemba 1678 Utawala wa Ufaransa.
Septemba 1678 (iliachwa na wote)
5 Oktoba 1685   - 7 Machi 1721 Utawala wa Brandenburg (tangu 1701 Prussia)
7 Machi 1721   - 11 Januari 1722 Utawala wa Ufaransa.
11 Januari 1722   - 20 Februari 1724 Utawala wa Uholanzi.
20 Februari 1724   - Machi 1728 Utawala wa Ufaransa.
tangu 1728   - Machi 1903 Utawala wa milki za Waberber
tangu 1903   - 28 November 1960 Utawala wa Ufaransa
tangu 28 November 1960 sehemu ya Jamhuri ya Mauritania

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]