Guruguru (familia)
Mandhari
Guruguru | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Guruguru koo-njano (Gerrhosaurus flavigularis)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Nusufamilia 2, jenasi 7:
|
Guruguru ni mijusi wa familia Gerrhosauridae walio na magamba magumu mgongoni. Mbavuni wana kunyanzi la ngozi kwa urefu mzima wa mwili.
Mwongoni mwa mijusi hawa kuna spishi kubwa kabisa za Afrika: hadi sm 75. Lakini nyingi ni sm 30-45. Mkia wa spishi za guruguru-nyoka (Tetradactylus) ni mrefu sana, zaidi ya mara mbili ya urefu wa mwili. Na miguu yao ni mifupi au haipo.
Huishi kati ya mawe na miamba, katika vishimo, katika vichuguu au takataka ya majani na matawi. Chakula chao ni wadudu hasa, kama panzi, mchwa na sisimizi, lakini majongoo, tandu, konokono na mijusi wengine pia, na spishi nyingine hula matunda na maua pia.
Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Broadleysaurus major, Guruguru Magamba-shupavu (Rough-scaled plated lizard)
- Gerrhosaurus flavigularis, Guruguru Koo-njano (Yellow-throated plated lizard)
- Gerrhosaurus nigrolineatus, Guruguru Mlia-mweusi (Black-lined plated lizard)
- Tetradactylus udzungwensis, Guruguru-nyoka wa Udzungwa (Udzungwa long-tailed seps)
- Zonosaurus madagascariensis insulanus, Guruguru-visiwa wa Shelisheli (Seychelles girdled lizard)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Guruguru magamba-shupavu
-
Guruguru mlia-mweusi
-
Guruguru-visiwa
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Guruguru (familia) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |