Fueli za kisukuku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Fueli ya kisukuku)
Rukia: urambazaji, tafuta
Makaa yanayowaka ni mfano wa fueli ya kisukuu

Fueli za kisukuku ni fueli kama makaa mawe, gesi asilia au mafuta ya petroli zilizotokana na mabaki ya mimea au miili ya bakteria, planktoni na wanyama katika mchakato ya miaka mingi sana.

Ndani yao kuna hasa hidrati kabonia au mata yenye hidrojeni na kaboni ndani yake.

Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Fueli za kisikuu zachomwa mara nyingi ama dani ya injini au kwa kupashia moto maji inayoendesha rafadha ya kutengeneza umeme.

Watu katika nchi za baridi huchoma pia fueli za kisukuu kwa kuwa na joto katika nyumba zao au kupika chakula.

Matumizi mengine ni mvevuko wa mafuta ya petroli au makaa kwa kupata fueli kama petroli, diseli au gesi za kuendesha injini mbalimbali.

Matatizo[hariri | hariri chanzo]

Kituo cha umeme kinapochomwa makaa nchini Poland

Fueli za kisukuu husababisha machafuko wa hewa wakati wa kuchimwa. Machafuko haya yachangia kwenye kupanda kwa halijoto duniani.

Pia fueli a kisukuu zinazidi kupungua haraka kwa sababu zilitokea katika muda wa miaka mamilioni lakini zinachomwa kwa kasi kubwa.

Wataalamu wengi huona ya kwamba akiba ya fueli za kisukuu zinaelekea kuishia katika miaka inayokuja karibuni. Hapo ndipo sababu ya kwamba wanatafuta njia ya kutumia nishati mbadala badala ya fueli za kisukuu.