Fransisko Coll

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Fransisko Coll.

Fransisko Coll (Gombren, 18 Mei 1812Vic, Barcelona, 2 Aprili 1875) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa Shirika la Wahubiri kutoka mkoa wa Catalonia, Hispania.

Baada ya kufukuzwa utawani kinyume cha haki, alidumisha imara wito wake akihubiri jina la Yesu katika mkoa huo wote.

Alianzisha shirika la Masista Wadominiko wa Kupashwa Habari Bikira Maria.

Tarehe 29 Aprili 1979 alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri, halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 11 Oktoba 2009.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Februari[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.