Nenda kwa yaliyomo

Fueli za kisukuku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Fossil fuel)
Makaa yanayowaka ni mfano wa fueli ya kisukuu

Fueli za kisukuku ni fueli kama makaa mawe, gesi asilia au mafuta ya petroli zilizotokana na mabaki ya mimea au miili ya bakteria, planktoni na wanyama katika mchakato ya miaka mingi sana.

Ndani yao kuna hasa hidrati kabonia au mata yenye hidrojeni na kaboni ndani yake.

Zinapatikana kutokana na mchakato unaobadilisha mata ya viumbehai kuwa kisukuku.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Fueli za kisukuku zachomwa mara nyingi ama dani ya injini au kwa kupashia moto maji yanayoendesha rafadha ya kutengeneza umeme.

Katika nchi za baridi watu huchoma pia fueli za kisukuku ili kuwa na joto katika nyumba zao au kupa chakula.

Matumizi mengine ni mvevuko wa mafuta ya petroli au makaa kwa kupata fueli maalumu kama petroli, diseli au gesi za kuendesha injini mbalimbali.

Matatizo

[hariri | hariri chanzo]
Kituo cha umeme kinachochoma makaa nchini Poland

Fueli za kisukuku husababisha machafuko ya hewa wakati wa kuchomwa. Machafuko hayo yanachangia kupanda kwa halijoto duniani.

Fueli za kisukuku zilijengwa katika vipindi vya miaka milioni kadhaa. Matumizi yao yalianza kuzidi tangu karne ya 19. Akiba zinazidi kupungua haraka kwa sababu zinachomwa kwa kasi kubwa.

Wataalamu wengi huona ya kwamba akiba ya fueli za kisukuku zinaelekea kuisha katika miaka inayokuja karibuni. Ndiyo sababu wanatafuta njia ya kutumia nishati mbadala badala ya fueli za kisukuku.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fueli za kisukuku kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.