Flaviano wa Roma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Flaviano na watakatifu wanawake wawili, mchoro wa ukutani, Montefiascone, Italia.
Mt. Flaviano juu ya farasi, mchoro wa ukutani, Montefiascone, Italia.

Flaviano wa Roma (aliuawa Montefiascone, 22 Desemba 361) alifia dini ya Ukristo katika dhuluma ya kaisari Juliano mwasi mwaka 361].

Inasemekana kwamba alikuwa mkuu wa jiji la Roma, lakini dhuluma ilipoanza tena alipaswa kumuachia cheo Aproniano, adui yake mkubwa na mfuasi wa dini ya jadi.

Kwa kuwa alikamatwa akizika wafiadini 3, alitiwa kwa moto alama ya watumwa na kupelekwa Aquas Taurinas (labda Montefiascone ya leo) afanye kazi ya shokoa, mpaka alipouawa tarehe 22 Desemba 361.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Desemba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Alban - Butler | Il primo grande dizionario dei santi secondo il calendario| 2001| Edizioni PIEMME S.p.A | Casale Monferrato|isbn= 88-384-6913-X
  • A. Cattabiani | Santi d'Italia, Volume secondo | Rizzoli| Milano | 2004 | isbn=88-17-00335-2
  • T. Vitaliano | La basilica di San Flaviano a Montefiascone. Restauri di affreschi: ipotesi | Ediart| 1987
  • M. Mari | Le reliquie del martire Flaviano | Centro iniziativeculturali| Montefiascone| 1991

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.