Nenda kwa yaliyomo

Flavi Klementi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Flavi Klementi (jina kamili kwa Kilatini: Titus Flavius T. f. T. n. Clemens, alifariki Roma, 95) alikuwa ndugu wa kaisari Domitian, na alikuwa konsuli wa Roma pamoja naye tangu Januari hadi Aprili mwaka 95 BK.

Muda mfupi baada ya kuacha kazi alihukumiwa adhabu ya kifo kama mkanamungu[1], tuhuma iliyotumiwa na Dola la Roma dhidi ya Wayahudi na Wakristo kwa kuwa walikataa ibada za miungu[2][3][4][5].

Anaheshimiwa na Wakristo kama mtakatifu mfiadini[6][7] sawa na mke wake Flavia Domitila.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Juni[8]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Grainger, Nerva and the Roman Succession Crisis of AD 96-99, p. 12.
  2. Cassius Dio, Roman History lxvii. 14.
  3. Philostratus, Life of Apollonius of Tyana, viii. 15.
  4. Eusebius, Historia Ecclesiastica, iii. 14.
  5. Jerome, Epistulae, 27.
  6. Dictionary of Greek and Roman Biography and Mythology, vol. I, p. 788 ("T. Flavius Clemens").
  7. http://www.santiebeati.it/dettaglio/92420
  8. Martyrologium Romanum
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Flavi Klementi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.