Eustolia na Sopatra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Eustolia na Sopatra (walifariki Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, karne ya 6) walikuwa mabikira Wakristo walioanzisha monasteri katika jiji hilo[1].

Eustolia alitokea Roma, Italia. Alipokwenda Konstantinopoli kutembelea makanisa alifahamiana na Sopatra, binti kaisari Maurisi, ambaye alimuomba awe mama yake ya kiroho na baada ya kifo chake alishika uongozi wa monasteri.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu.

Sikukuu yao inaadhimishwa hasa tarehe 9 Novemba[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.