Erling Braut Håland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
haaland akicheza dhidi ya wolfsburg
Haland akiwa na mpira.

Erling Braut Haaland (alizaliwa 21 Julai 2000) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Norway ambaye anacheza kama mshambuliaji wa klabu ya Ujerumani Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Norway.

Håland alianza kazi yake katika klabu ya nyumbani kwake Bryne FK mnamo 2016, na alihamia Molde FK mwaka uliofuata ambapo alitumia miaka miwili. Mnamo Januari 2019 alihamia upande wa Austria Red Bull Salzburg kwa mkataba wa miaka mitano. Alicheza katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya (UEFA) ya 2019-20, alikuwa kijana mdogo kuliko wote kucheza mechi tano mfululizo za Ligi ya Mabingwa ya UEFA.

Mnamo 29 Desemba 2019, Håland alihama kwenda Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa ada iliyoripotiwa kuwa milioni 20.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Erling Braut Håland kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.