Nenda kwa yaliyomo

Elizabeti wa Ureno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Elizabeti wa Ureno alivyochorwa na José Gil de Castro, 1820 (Santiago, Cile).
Mt. Isabela wa Aragona.
Muujiza wa mawaridi ulivyochorwa na Valerio Castello, 1650 hivi.
Sanduku lake la mwaka 1330, katika kanisa la Mt. Klara huko Coimbra.
Mchoro wa Petrus Christus, 1460 hivi, ukimuonyesha Mt. Isabela wa Aragona na jamaa yake Mt. Elizabeti wa Hungaria.

Elizabeti wa Ureno (anayejulikana pia kama Isabela Perez au Isabela wa Aragona; Saragoza, Hispania, 4 Januari 1271 - Estremoz, Ureno, 4 Julai 1336) alikuwa malkia wa nchi hiyo (1282-1325) kabla hajaanzisha jumuia ya kimonaki ya Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko karibu na monasteri ya Waklara.

Aling'aa kwa juhudi za kuleta upatanisho kati ya wafalme na kusaidia maskini akafariki wakati wa kushughulikia amani kati ya mwanae na mkwe wake[1]

Alitangazwa na Papa Urban VIII kuwa mtakatifu tarehe 25 Mei 1625.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/28050
  2. Martyrologium Romanum

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Ferreira, João (2010), Histórias Rocambolescas da História de Portugal (toleo la 6), Lisbon, Portugal: A Esfera dos Livros, ISBN 978-989-626-216-7 {{citation}}: Unknown parameter |trans_title= ignored (|trans-title= suggested) (help)
  • Hoever, Hugo, mhr. (1955), Lives of the Saints, For Every Day of the Year, New York, New York: Catholic Book Publishing Co., uk. 511

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.