Elimu madini
Elimu madini (kwa Kiingereza: mineralogy) ni tawi la jiolojia linalochunguza kemia, muundo na tabia za madini.
Madini ni vitu ambavyo huunda miamba. Kuna aina nyingi tofauti za madini. Baadhi ni ngumu, kama almasi. Baadhi ni laini, kama jasi. Baadhi ni metali, kama dhahabu au chuma.
Madini hupangwa katika vikundi maalum kulingana na kemikali ndani yake, au kulingana na muundo za fuwele ndani yake.
Uchunguzi wa madini unaleta habari nyingi kuhusu miamba na historia ya Dunia. Elimu hiyo inasaidia pia kuelewa nafasi kwa matumizi ya madini tofauti, na kuongoza utafiti kwa kupata madini mbadala au kutengeneza madini kwenye maabara kwa matumizi katika teknolojia.
Wakati mwingine sura au umbo la madini vinaonyesha jinsi yalivyoundwa. Kwa mfano, madini katika miamba ya mgando (igneous rock) yanasaidia kujua umri wa mwamba tangu kuganda (kubadilika kutoka lava kuwa mwamba). Madini makubwa yanamaanisha mwamba uliopozwa polepole (labda chini ya ardhi). Madini madogo humaanisha kuwa mwamba ulipozwa haraka (labda juu ya ardhi, kama kutoka volkeno). Aina za madini katika mwamba pia zinaweza kuonyesha ni mwamba wa aina gani, au kile kilichotokea kwa mwamba tangu kuundwa. Miamba mingi hupewa jina kulingana na aina ya madini iliyonayo.
Wataalamu wa elimu madini huangalia madini katika miamba kwa kutumia lenzi za mkononi, na kwa undani zaidi wakikata mabapa membamba na kuyachungulia chini ya hadubini. Huangalia umbo na ukubwa wa fuwele, na rangi ya madini. Maelezo hayo yanasaidia kujua ni madini gani yanayoangaliwa.
Madini hutumika katika mambo mengi tofauti, kama mapambo ya vito, kilimo, ufinyanzi, kutengeneza metali na mengine.
Tovuti za Nje
[hariri | hariri chanzo]- International Mineralogical Association
- Mineralogical Association of Canada
- Virtual Museum of the History of Mineralogy Ilihifadhiwa 28 Aprili 2010 kwenye Wayback Machine.
- Geological Society of America Ilihifadhiwa 18 Januari 2022 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Elimu madini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |