Nenda kwa yaliyomo

Egbert wa Ripon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Egbert wa Ripon (jina asili: Ecgberht; 639 - 729) alikuwa mmonaki, halafu askofu wa Lindisfarne[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Ecgberht alikuwa sharifu wa Kigermanik wa Northumbria.[2] Mwaka 664, akiwa kijana, alikwenda kusoma katika monasteri ya Ireland.[3] Huko alimfahamu Chad wa Mercia.[4]

Alipopatwa na tauni akiwa na umri wa miaka 25 aliweka nadhiri ya kufanya daima toba nje ya nchi yake[2]. Kisha kupona alitimiza alichoahidi hadi alipofariki akiwa na miaka 90.[5]

Pia aliandaa wamonaki wengi kwenda kuinjilisha Frisia (Uholanzi) ila mwenyewe alizuiwa.[6] [5]

Mwaka 684 alijaribu kumzuia mfalme Ecgfrith wa Northumbria asipeleke jeshi lake dhidi ya Ireland.[7]

Mwaka 697 alishiriki sinodi ya Birr iliyopitisha Cáin Adomnáin ili kutetea usalama wa raia.[8]

Mwaka 716 alihimiza wafalme wa Northumbria na wa Wapiti, na pia monasteri ya Iona, wakubali tarehe ya Pasaka kadiri ya kalenda ya Kanisa la Roma[9] naye alifariki Iona[10] tarehe 24 Aprili 729, iliyokuwa siku ambapo Pasaka iliadhimishwa huko kwa mara ya kwanza kadiri ya kalenda hiyo.[11]

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Wakatoliki na Waorthodoksi wanaadhimisha sikukuu yake tarehe ya kifo chake, 24 Aprili. [12][13]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.