Nenda kwa yaliyomo

Edward Steere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Edward Steere

Amekufa 26 Agosti 1882
Kazi yake mwanatheolojia]
Cheo Askofu


Edward Steere (1828 - 26 Agosti 1882) alikuwa mwanatheolojia Mwanglikana kutoka Uingereza aliyepata kuwa askofu wa Zanzibar akikumbukwa kuwa kati ya Wazungu wa kwanza waliokusanya matini za Kiswahili na kutunga sarufi ya lugha hiyo. [1]

Steere alisoma theolojia kwenye Chuo Kikuu cha London akabarikiwa mnamo 1850. [2] Baada ya kuhudumia kama mchungaji huko Devon na Lincolnshire, alijiunga na William Tozer (Askofu Mwanglikana wa Afrika ya Kati) kwenye safari ya kwenda Unyasa mnamo 1863. [3] Aliteuliwa Askofu wa Afrika ya Kati [4] mnamo 1874 akaaga dunia mnamo 26 Agosti 1882. [5]

Edward Steere alikaa miaka mingi kule Zanzibar, 1864-1868, 1872-1874, na 1877-1882. Mnamo 1873 aliweka jiwe la msingi katika Kanisa la Christ Church, Zanzibar, katika Mji Mkongwe wa Unguja. Alishiriki katika ubunifu wa kanisa hilo lililojengwa mahali pa soko la watumwa la awali. Steere alishirikiana pia na David Livingstone kwa lengo la kumaliza utumwa huko Zanzibar. Amezikwa nyuma ya madhabahu kwenye kanisa. [6]

Mnamo mwaka 1875 alianzisha shirika lifaamikalo kama "The East Africa Church Missionary Society" (EACMS) ambalo lilitoa mafunzo kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Askofu Edward Steere pamoja na shirika lake waliweza kuanzisha kamusi mbalimbali. Kwa uzuri zaidi shirika hilo ndilo lililosanifisha lugha ya Kiswahili mnamo mwaka 1930.

Mtafiti wa lugha

[hariri | hariri chanzo]

Steere alikuwa mtaalamu mkubwa wa lugha akatoa vitabu kadhaa kuhusu lugha mbalimbali za Afrika Mashariki, zikiwa pamoja na Kishambala, Kiyao, Kinyamwezi, na Kimakonde. Lakini anafahamika zaidi kwa utafiti wake kuhusu Kiswahili. Alitunga "Handbook of Swahili" (Mwongozo wa Kiswahili) mnamo 1870, alipojumlisha sarufi pamoja na kamusi ndogo. Pia alikusanya masimulizi aliyosikia Unguja (Swahili Tales) na kutafsiri sehemu kubwa ya Biblia. [7] Mwanafunzi wake A.C. Madan alitumia kazi ya Steere alipoendelea kutunga kamusi za Kiswahili-Kiingereza na Kiingereza-Kiswahili zilizokuwa kamusi sanifu kwa miaka mingi.

Vitabu alivyotunga

[hariri | hariri chanzo]
  • Steere, Edward. 1869. Anjili ya Bwana Wetu na Mwokozi Wetu Isa Masiya kwa

Mattayo. Maneno ya Kiswahili. London.

  • Steere, Edward. 1870. Handbook of the Swahili Language, as spoken at Zanzibar.

London. Bill & Dadly. (B.8.17.11.).

  • Steere, Edward. 1876. On the Use of Arabic Alphabet in Swahili. UMCA.
  • Steere, Edward. 1882. Swahili Exercises Compiled for the Universities´ Missions to

Central Africa. London.

  • Steere, Edward. 1906. Swahili Tales. London: Bell & Dadly (Revised 1922: London, SPCK
  1. Zanzibar Christians
  2. The Times, Tuesday, Aug 29, 1882; pg. 6; Issue 30598; col D Obituary
  3. Heanley, R. M. A Memoir of Edward Steere, D.D. Ll.D., Third Missionary Bishop in Central Africa. (see External links).
  4. Ranger, Terence O.; Kimambo, Isaria N. (1976). The Historical Study of African Religion. University of California Press. ISBN 978-0-520-03179-1.
  5. The Times, Tuesday, Sep 19, 1882; pg. 4; Issue 30616; col F Bishop Steere And His Work
  6. 'Workers at the church'
  7. Dictionary of National Biography entry; see External links below.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.