Nenda kwa yaliyomo

Edith Masai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rekodi za medali
Women's Wanariadha
Anawakilisha nchi Bendera ya Kenya Kenya
World Cross Country Championships
Medali ya Shaba 2001 Ostend Short race
Dhahabu 2002 Dublin Short race
Dhahabu 2003 Lausanne Short race
Dhahabu 2004 Brussels Short race
World Championships
Medali ya Shaba 2003 Paris 5000 m
African Championships in Athletics
Dhahabu 2006 Bambous 10000 m
Michezo ya Afrika Nzima
Fedha 2007 Algiers 10000 m

Edith Chewangel Masai (alizaliwa mnamo 4 Aprili 1967) ni mwanariadha kutoka Kenya. Mafanikio yake bora ni medali tatu za dhahabu za kibinafsi katika mashindano ya dunia ya kuvuka nchi ya IAAF kati ya mwaka wa 2002 na 2004. Pia anajulikana kwa kufikia mpaka wa kimataifa akiwa na umri wa miaka 35.

Wasifu wa Mapema

[hariri | hariri chanzo]

Masai alizaliwa katika kijiji cha Chepkoya, wilaya ya Mlima Elgon. Alishindana wakati wake wa shule ya sekondari wakati alikuwa katika shule ya upili ya Kibuk. Alihitimlu kutoka skuli hiyo mwaka wa 1988. Alijiunga na Kenya Prisons Service mwaka wa 1990, inayojulikana sana kwa kusajili wanariadha wengi wenye vipaji. Masai hata hivyo, hakupata chochote hadi mwaka wa 1999, wakati akawa bingwa wa mbio za kuvuka nchi au “cross-county” ukipenda,akiwa na umri wa miaka 32. Baada ya ushindi huu, alianza kufanya mazoezi zaidi kwa umakini

Wasifu wa Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Masai anashikilia rekodi ya Afrika ya mita 3,000 iliyowekwa mnamo Julai 2002 katika mji mkuu wa Monako.

Edith alishinda medali ya shaba katika mashindano ya dunia ya mwaka wa 2003. Mwaka wa 2004 alishindwa katika majaribio ya Kenya kushiriki katika michezo ya Olimpiki, lakini tangu alikuwa mmoja wa Wakenya watatu tu ambao walikuwa wameishinda wakati wa kufuzu wa Olimpiki "A"- katika mbio ya mita 5000 ya wanawake mwaka huo, alipewa nafasi kwenye timu. Masai mwenyewe awali alikuwa ameikataa fursa hiyo, lakini alijiunga na timu baada ya mazungumzo marefu. Katika Michezo ya Olimpiki alijiondoa mashindanoni kwa kulalamikia jeraha la “hamstring”.

Edith alimaliza katika nafasi ya 5 katika mbio za mita 10000 katika mashindano ya dunia yaliyofanyika katika mji mkuu wa Helsinki mwaka wa 2005 nchini Finland. Muda wake wa dakika 30:30.26 ulikuwa rekodi mpya ya Kenya Rekodi hiyo ilivunjwa na Linet Masai katika Michezo ya Olimpiki mwaka wa 2008, ambaye alikimbia kwa muda wa dakika 30:26.50

Tangu wakati huo Masai ameacha kukimbia mbio za “track” na ameanza kukimbia mbio za marathon. Masai alishinda Marathon ya Hamburg mwaka wa 2005 na alishiriki katika marathon hiyo katika miaka ya 2006 na 2007. Mwaka wa 2006 aliibuka mshindi katika marathon nusu ya Berlin, kuweka muda wa kasi zaidi katika nusu marathon iliyokimbiwa mwaka huo, dakika 1:07:16. Pia ilikuwa muda bora wa kibinafsi na rekodi ya kozi. Pia aliweka rekodi mpya ya Kenya ya mita 5000 kwa muda wa dakika 14:33.84.

Edith alishinda medali ya fedha katika mbio ya mita 10000 katika Michezo ya All-Africa mwaka wa 2007. . Muda wake wa dakika 31:31.18 ni rekodi mpya ya Dunia kwa mwanamke aliye na umri zaidi ya miaka 40. Rekodi ya hapo awali ilikuwa inashikiliwa na Nicole Leveque wa Ufaransa, ambaye alikimbia kwa muda wa dakika 32:12.07 katika mji mkuu wa Helsinki mwaka wa 1994. Masai alishiriki katika marathon ya mashindano ya dunia mwaka wa 2008 katika mji mkuu wa Osaka nchini Japani, na kumaliza katika nafasi ya 8 katika mbio ambayo ilishindwa na mkimbiaji mwenzake Catherine Ndereba.

Masai alishinda mbio ya nusu marathon ya Rock 'n' Roll ya mwaka wa 2008 katika ufukoni mwa Virginia, VA. Edith alishinda Marathon ya Singapore mnamo Desemba 2008.

Kwa sasa yeye anaishi katika mji mkuu wa Nairobi na Trier, Ujerumani. Yeye ni talaka. Yeye ni mama wa mvulana, aliyezaliwa mwaka wa 1990. Yeye hufanyishwa mazoezi na Dorothee Paulmann.

Mwaka Mchuano Ukumbi Tokeo Muda Maelezo
2001 Mashindano ya Dunia ya XC Ostend, Ubelgiji 3 x Mbio fupi
2 x Mbio fupi ya Timu
Mashindano ya Dunia Edmonton, Kanada 7 15:17.67 mita 5000
Fainlali ya Grand Prix Melbourne, Australia 7 x mita 3000
2002 Mashindano ya Dunia ya XC Dublin, Ireland | [1] x Mbio fupi
2 x Mbio fupi ya Timu
Michezo ya Jumuiya ya Madola Manchester, Uingereza 2 x mita 5000
Fainali ya Grand Prix Paris, Ufaransa 4 x mita 3000
2003 Mashindano ya Dunia ya XC Lausanne, Uswisi | [1] x Mbio fupi
| [1] x Mbio fupi ya timu
Mashindano ya Dunia Paris, Ufaransa 3 14:52.30 mita 5000
Fainali za mbio za dunia Monako | [1] x mita 3000
2004 Mashindano ya Dunia ya XC Brussels, Ubelgiji | [1] x Mbio fupi
2 x Mbio fupi ya timu
Fainali za mbio za dunia Monako 4 x mita 5000
2005 Mashindano ya Dunia Helsinki, Finland 5 x mita 10000
Fainali za mbio za dunia Monako 6. x mita 3000
2006 Mashindano ya Kiafrika Bambous, Mauritius | [1] x mita 10000
Mashindano ya kukimbia ya barabara ya dunia Debrecen, Hungaria 5 x
| [1] x Mbio ya timu
Fainali za mbio za dunia Stuttgart, Ujerumani 7 x mita 5000
2007 Michezo ya All-Africa Alger, Algeria 2 x mita 10000
Mashindano ya Dunia 2007 Osaka, Japan 8 x Marathon

Ubora wa kibinafsi

[hariri | hariri chanzo]
Umbali. Muda Mji Tarehe
mita 3000 8:23.23 Monako 19 Julai 2002
mita 5000 14:33.84 Oslo 2 Juni 2006
mita 10,000 30:30.26 Helsingfors 6 Agosti 2005
Kilomita 10 31:13 La Courneuve 31 Machi 2002
Kilomita 15 47:52 Berlin 2 Aprili 2006
Kilomita 20 1:03:52 Berlin 2 Aprili 2006
Nusu Marathon 1:07:16 Berlin 2 Aprili 2006
Kilomita 30 1:42:15 Hamburg 23 Aprili 2006
Marathon 2:27:06 Hamburg 24 Aprili 2005
Kilomita 5 14:50 Neuss 8 Juni 2002
Maili 10 ya barabara 52:45 Zaandam 22 Septemba 2002


Sporting positions
Alitanguliwa na
Kenya Emily Kimuria
Mshindi wa Marathon ya Hamburg
2005
Akafuatiwa na
Ethiopia Robe Tola