Diego wa Alkala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mtakatifu Diego
Mt. Diego akiwa ametoka nje ya nafsi yake mbele ya msalaba mchoro wa Murillo, 1645-6

Diego wa Alkala alikuwa bruda wa shirika la Ndugu Wadogo; anashimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Alifanya kazi ya umisionari katika visiwa vya Kanaria (karibu na pwani wa Moroko).

Alipohiji Roma kwa Jubilei alijitosa kuhudumia waliopatwa na tauni.

Alizaliwa mwaka 1400 hivi huko San Nicolás del Puerto (Hispania), akafa tarehe 12 Novemba 1463 huko Alcalá de Henares (Hispania).

Alitangazwa mtakatifu na Papa Sixtus V mwaka 1588. Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Novemba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]