Deogratias wa Karthago

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Deogratias wa Karthago[1][2] alikuwa askofu wa mji huo (katika Tunisia ya leo) katika miaka 454 - 457[3].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[4] .

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Januari na 22 Machi[5][6][7].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Inawezekana ni mtu yuleyule aliyetajwa mara nne na Augustino wa Hippo katika maandishi yake kama shemasi Deogratias halafu kama padri Deogratias[8].

Kutokana na dhuluma za Wavandali[9], kabla yake jimbo la Karthago lilikaa bila askofu miaka 14 tangu alipofariki Quodvultdeus na baada yake kwa miaka 23 tena hadi alipoteuliwa Eugenius wa Karthago[10][11][12]..

Deogratias aliuza vitu vyote vya thamani vya Kanisa ili kukomboa waliokuwa wametekwa na Wavandali kama watumwa mjini Roma akawalaza na kuwalisha katika mabasilika mawili.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]