Denis Mukwege

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Denis mwaka 2014.

Denis Mukwege (alizaliwa Bukavu, katika Kongo ya Belgiji, leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, 1 Machi 1955) ni daktari na mchungaji wa kanisa la Kipentekoste. Yeye ni maarufu kwa sababu alishinda Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka wa 2018 kwa kazi yake ya kusaidia wanawake ambao ni waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia.[1]

Maisha ya utotoni[hariri | hariri chanzo]

Yeye ni mtoto wa tatu. Yeye ana ndugu wengine wanane. Baba yake ni mchungaji wa Kipentekoste kama yeye. Baada ya kumwangalia baba yake akiwaombea watu wengi wagonjwa, yeye alinuia kuwa daktari.[2] Yeye alitaka kuwasaidia wanawake ambao walikuwa wajawazito na hawakuweza kupata madaktari wenye utaalam.

Elimu na shughuli[hariri | hariri chanzo]

Elimu yake ni Shahada ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu Cha Burundi, Shahada ya jinakolojia na uzazi kutoka Chuo Kikuu Cha Angers, na Shahada ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu Cha Brussels.[3]

Denis alikwenda Burundi na yeye alipokea Shahada ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu Cha Burundi. Alirudi mji wa Bukavu na alifanya kazi katika Hospitali ya Lemera. Lakini, yeye alirudi shuleni kwa sababu yeye aliona hakukuwa na huduma za kutosha kwa wagonjwa wa kike. Alipokea Shahada ya jinakolojia na uzazi kutoka Chuo Kikuu Cha Angers katika nchi ya Ufaransa mwaka wa 1989 na aliendelea kufanya kazi kwa Hospitali ya Lemera.[4]

Baada ya Vita vya Kwanza vya Kongo, Denis alianzisha Hospitali ya Panzi mwaka wa 1999. Imetibu wagonjwa zaidi ya 82,000. Zaidi ya 60% ya wagonjwa hao ni waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia kutokana na vita katika kanda.[5] Kwa kazi hio, alitajwa kama “Mwafrika wa Mwaka” katika mwaka wa 2009.[6]

Hotuba ya Umoja wa Mataifa (UN) na Jaribio la Mauaji[hariri | hariri chanzo]

Mwezi tisa mwaka 2012, yeye alizungumza katika UN kuhusu na unyanyasaji wa kijinsia katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yeye alisema kuwa serikali ya Kongo na nchi nyingine wanahitaji kusaidiwa kuacha vita kwa sababu unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake ni ilitumika kama silaha ya vita.[7]

Tarehe 25 Oktoba 2012, wanume wanne na bunduki waliingia katika nyumba ya Denis na walishika binti zake mateka. Aliporudi nyumbani, wao walijaribu kumuua Denis lakini walishindwa. Denis alikwenda uhamishoni katika Ulaya, lakini mwaka 2013 yeye alirudi nchini ya Kongo na watu wengi walimsalimia yeye kwa furaha.[8]

Tuzo la Amani la Nobel[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 2018, Denis Mukwege alishinda Tuzo la amani la Nobel na Nadia Murad. Yeye alishinda kwa kazi yake ya kuhusu unyanyasaji wa kijinsia kama silaha ya vita. Yeye amesaidia maelfu ya waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia na alitangaza kuwa wahalifu wote walifaa kuhukumiwa.[9]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  1. "The Nobel Peace Prize 2018". NobelPrize.org (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-07-26. 
  2. "Dr. Denis Mukwege". Panzi Foundation (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-07-26. 
  3. "Denis Mukwege", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-07-22, iliwekwa mnamo 2019-07-26 
  4. "Denis Mukwege", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-07-22, iliwekwa mnamo 2019-07-26 
  5. Where repairing rape damage is an expertise, iliwekwa mnamo 2019-07-26 
  6. Denis Mukwege - 'Dr Miracle' (kwa en-GB), 2018-10-05, iliwekwa mnamo 2019-07-26 
  7. "Dr. Denis Mukwege". Panzi Foundation (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-07-26. 
  8. "Dr. Denis Mukwege". Panzi Foundation (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-07-26. 
  9. "The Nobel Peace Prize 2018". NobelPrize.org (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-07-26.