Nenda kwa yaliyomo

Chuo Kikuu cha Marburg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chuo Kikuu cha Marburg (kwa Kijerumani: Philipps-Universität Marburg) ilianzishwa mwaka wa 1527 na Philip I, mtemi wa Hesse. Ni kimojawapo cha vyuo vikuu vya kale zaidi vya Ujerumani. Kilianzishwa kama chuo kikuu cha Kiprotestanti miaka michache baada ya matengenezo ya Martin Luther. Sasa ni chuo kikuu cha umma cha jimbo la Hesse, bila tabia ya kidini.

Chuo Kikuu cha Marburg kina wanafunzi wapatao 23,500 na wafanyakazi 7,500. Kiko katika mji wa Marburg wenye wakazi 76,000; hivyo wanafunzi na waajiriwa wa chuo kikuu ni sehemu muhimu ya uchumi wa mji wote. Majengo ya chuo kikuu yamesambaa kote kwenye mji.

Karibu asilimia 14 za wanafunzi si Wajerumani ambayo ni asilimia kubwa zaidi ya wanafunzi wa kimataifa nchini Hesse. [1]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Wahitimu mashuhuri na kitivo[hariri | hariri chanzo]

Wataalamu wa sayansi asilia[hariri | hariri chanzo]

 

Wanatheolojia[hariri | hariri chanzo]

Marburg ilijulikana tangu mwanzoni kama chuo kikuu kinachozingatia sayansi za jamii. Ilihifadhi umaarufu huo hasa katika falsafa na theolojia kwa muda mrefu baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia .

 

Wanafalsafa[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Uni International – Philipps-Universität Marburg". Iliwekwa mnamo 21 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)