Nenda kwa yaliyomo

Nyigu-kekeo (Chrysididae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Chrysis)
Nyigu-kekeo
Nyigu-zumaridi (spishi isiyotambuliwa)
Nyigu-zumaridi (spishi isiyotambuliwa)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno kipana)
Familia ya juu: Chrysidoidea
Familia: Chrysididae
Nusufamilia: Chrysidinae
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Makabila 5:

Nyigu-kekeo au nyigu-zumaridi (kutoka kwa Kiing. cuckoo wasps au emerald wasps) ni nyigu wadogo wa nusufamilia Chrysidinae katika familia Chrysididae ya oda Hymenoptera walio na rangi zinazong'aa kama johari, k.m. kijani, buluu na nyekundu. Nyigu hawa hawachomi. Kama vile kekeo, majike hutaga mayai yao katika viota vya nyuki na nyigu wapweke, ambayo ni asili ya jina lao la kwanza. Walipata jina lao la pili kwa sababu spishi za kwanza zilizojulikana sana zilikuwa kijani kama zumaridi kabisa au kwa sehemu kubwa. Spishi zilizo na fumbatio nyekundu huitwa nyigu mkia-yakuti pengine (jina lisilo sahihi sana).

Hawa ni nyigu wadogo wenye urefu wa mm 3-22, ingawa mara chache huzidi mm 12. Wana kiunzi nje kigumu sana. Pingili tatu tu zinaonekana kwenye fumbatio[1]. Mabamba ya mgongo ya pingili hizi hujipinda na kuficha mabamba ya tumbo zisionekane kutoka upande. Mabamba ya tumbo ni bapa au mbonyeo[2]. Pingili nyingine zimerudishwa ndani ya mwili na kuunda neli za uzazi. Neli ya kutagia hutumika tu kwa kutaga mayai na sio kwa kuchoma[3]. Nyigu-kekeo wana rangi angavu, haswa kijani, buluu na nyekundu, ambazo hutokea peke yao au kwa michanganyiko. Zinang'aa kama zumaridi, zabarijadi na yakuti.

Biolojia

[hariri | hariri chanzo]

Nyigu-kekeo ni vidusia wa nyigu na nyuki wapweke[3]. Majike huingia katika mashimo ya viota ambapo hutaga yai karibu na kila yai au buu la kidusiwa. Kisha buu anayeibuka hula buu kidusiwa au, katika spishi nyingine, kwanza buu kidusiwa akiwa bado mdogo, na kisha chakula kilichotolewa na mdudu kidusiwa[3]. Jike hulindwa dhidi ya kidusiwa aliyekasirika kwa kiunzi nje kigumu na kwa tabia yake ya kujiviringa katika tufe ili kulinda miguu yake na sehemu za chini za kichwa[4].

Spishi za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]
  • Chrysis alternans
  • Chrysis andromeda
  • Chrysis angolensis
  • Chrysis antennate
  • Chrysis aurifascia
  • Chrysis campanai
  • Chrysis capitalis
  • Chrysis cincta
  • Chrysis delicatula
  • Chrysis dira
  • Chrysis heymonsi
  • Chrysis jousseaumei
  • Chrysis kenyana
  • Chrysis laborans
  • Chrysis laeta
  • Chrysis laminata
  • Chrysis lesnei
  • Chrysis macrodon
  • Chrysis maindroni
  • Chrysis mandibularis
  • Chrysis mediocris
  • Chrysis munita
  • Chrysis nasuta
  • Chrysis nidicola
  • Chrysis pachysoma
  • Chrysis pachystoma
  • Chrysis palliditarsis
  • Chrysis plagiata
  • Chrysis postscutellaris
  • Chrysis rutilata
  • Chrysis salamensis
  • Chrysis schoenherri
  • Chrysis scutata
  • Chrysis semifumata
  • Chrysis tesserops
  • Chrysis ugandae
  • Chrysis ugandana
  • Chrysis verudens
  • Chrysis voiensis
  • Chrysis zanzibarica
  • Odontochrydium bicristatum
  • Odontochrydium irregulare
  • Odontomutilla inversa
  • Praestochrysis clotho
  • Praestochrysis gaullei
  • Praestochrysis guineae
  • Praestochrysis inops
  • Praestochrysis leechi
  • Praestochrysis nigromaculata
  • Praestochrysis pentodontophora
  • Praestochrysis septidens
  • Primeuchroeus ghilianii
  • Stilbum cyanurum
  • Trichrysis eardleyi
  • Trichrysis polinierii
  1. Torretta, J.P. (2015). "Host–parasite relationships and life cycles of cuckoo wasps in agro-ecosystems in Argentina (Hymenoptera: Chrysididae: Chrysidini)". Journal of Natural History. 49 (27–28): 1641–1651. doi:10.1080/00222933.2015.1005710. S2CID 84594440.
  2. Lucena, D.; Kimsey, L.S.; Almeida, E. (2019). "Phylogenetic relationships and biogeography of the Ipsiura cuckoo wasps (Hymenoptera: Chrysididae)". Systematic Entomology. 44 (1): 192–210. doi:10.1111/syen.12320. S2CID 92508094.
  3. 3.0 3.1 3.2 Kimsey, L.S. (2006). "California cuckoo wasps in the family Chrysididae (Hymenoptera)". {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)
  4. Triplehorn, C.A.; Johnson, N.F.; Borrow, D.J. (2005). Borrow and DeLong's Introduction to the Study of Insects.