Nenda kwa yaliyomo

Samaki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Cephalaspidomorphi)

Kuhusu kundinyota la Pisces linaloitwa pia "Samaki" angalia hapa

Samaki
Kundi la tengesi mkia-njano (Sphyraena flavicauda)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Faila ya chini: Gnathostomata (Wanyama wenye mataya)
Ngazi za chini

Kladi 5 za samaki:

Papa buluu.

Samaki ni wanyama wenye damu baridi wanaoishi kwenye maji ya mito, mabwawa, maziwa au bahari.

Wote ni vertebrata, yaani huwa na uti wa mgongo.

Wanatumia oksijeni iliyomo ndani ya maji kwa kuyavuta kwenye mashavu yao.

Kuna aina nyingi za samaki wadogo wenye urefu wa sentimita moja na wakubwa wenye urefu hadi mita 15. Ila tu viumbehai wakubwa kwenye maji si samaki bali nyangumi ambao ni mamalia.

Samaki na watu

Samaki ni viumbe wa ajabu.

Samaki ni chakula bora kwa sababu nyama yake ina protini nyingi inayopokewa kwa urahisi na mwili wa binadamu. Leo hii ni zaidi ya watu bilioni moja wanaotegemea samaki hasa kama chanzo cha protini.

Tangu zamani samaki walivuliwa na watu. Wanaoishi karibu na bahari au mito mikubwa mara nyingi ni wavuvi. Mbali ya samaki ambao hutegwa na watu kwa lengo la kula, kuna uvuvi wa michezo ambayo huenea duniani kote. Kuna njia mbili:

  • Njia ya jadi inajumuisha uwezo wa kukamata samaki kwa zana ambazo zinafanywa na mtu binafsi kama fimbo na ndoana
  • Njia ya kisasa iko leo katika uchumi wa magharibi, ambapo vifaa huuzwa na maduka ya uvuvi.

Mbali na kuvua tu, watu wanafuga pia samaki. Ufugaji samaki hutokea hasa katika mabwawa madogo; samaki wanapewa lishe ili wale na baada ya kufikia ukubwa unaotakiwa maji yanaondolewa kwenye bwawa. Lakini miaka ya nyuma ufugaji samaki umeenea hadi baharini. Vizimbi vikubwa vinatengenezwa kwa seng'enge na kuzamishwa katika sehemu ya bahari pasipo hatari ya mawimbi makali, kwa mfano katika hori nyembamba kama fyord za Norwei.

Samaki wanafugwa pia kama mapambo na kwa burudani: watu wanajua wale wenye rangi za pekee na kuwafuga hasa.

Vyakula anavyokula samaki

Faida za samaki katika jamii

Hutusaidia kula hata kuondoa janga la njaa katika sehemu fulani.

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Samaki kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.