Córdoba, Hispania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kitovu cha kihistoria ya Cordoba pamoja na mesqita
Ndani ya Mesqita ya Cordoba

Cordoba (Kihispania: Córdoba tamka kor-do-ba) ni mji wa wa kihistoria ya Andalusia katika kusini ya Hispania kando la mto Guadalquivir. Ni makao makuu ya mkoa wa Cordoba. Kuna wakazi 321,000.

Kwa jina la Corduba ilikuwa mji mkubwa wa Hispania kusini wakati wa Dola la Roma. Tangu karne ya 3 ilikuwa makao ya askofu. Askofu Ossius wa Corduba alishirika katika Mtaguso wa Nikea. Baadaye mji ulikuwa sehemu ya falme za Wavisigothi na Bizanti.

711 mji ulivamiwa na Waarabu Waislamu ukawa mji mkuu wa utemi na baadaye Ukhalifa wa Wamuawiya wa Cordoba. Wakati wa ukhalifa mji ukaitwa Qurtuba (Kar.'قرطبة') ulikuwa na wakazi milioni nusu ilikuwa kati ya miji mikubwa duniani ya karne yake. Wakazi walikuwa mchanganyiko wa Wakrsto, Waislamu na Wayahudi.

Baada ya mwisho wa ukhalifa wa Cordoba mji ulivamiwa na majirani malimbali ukawa chini ya utawala wa Waabadiya wa Sevilla, tangu 1069 chini ya Wamurabitun kutoka Moroko na Wamuwahidun. 1236 jeshi la Wakristo kutoka Hispania kaskazini likateka mji likabaki chini ya utawala wao na kuwa sehemu ya Hispania ya Kikristo.

Kati ya majengo ya kihistoria kuna

  1. Mezquita de Cordoba iliyoanzishwa 785 na Emir Abd ar Rahman kama msikiti uliopanushwa mara kadhaa hadi kufunika eneo la 23,000 . 1236 ilibadilishwa kuwa kanisa kuu ka mji.
  2. Daraja la Kiroma lilijengwa na Waroma wa Kale mwaka 45 likatengenezwa na kuimarishwa na Waaabu na Wahispania.

Pamoja na majengo mengine yamepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.