Bernard Kamilius Membe
Bernard Kamilius Membe (Rondo, Chiponda, Wilaya ya Lindi Vijijini, 9 Mei 1953 - Dar es Salaam, 12 Mei 2023) alikuwa mwanasiasa wa Tanzania aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimaitaifa chini ya rais Jakaya Kikwete pamoja na kuwa mbunge wa jimbo la Mtama katika bunge la kitaifa.[1][2] Mwaka 2016 alitaka kugombea urais kwa tiketi ya chama cha CCM akashindwa kupata nafasi.
Mnamo 2018 alilaumiwa katika gazeti la Tanzanite kuwa alijaribu kumzuia rais John Magufuli asipewe nafasi ya kugombea tena mwaka 2020. Membe alifungua kesi ya machafuko jina dhidi ya gazeti na mhariri wake.
Mwaka 2019 Membe aliitwa mbele ya kamati kuu ya CCM na kuhojiwa kuhusu mashtaka ya kula njama dhidi ya rais[3] akafukuzwa katika chama.
Baada ya kufukuzwa katika chama hicho alihamia chama cha ACT Wazalendo akawa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2020. Katika kampeni alionyesha juhudi kidogo tu. Baada ya uchaguzi aliondoka tena katika ACT [4].
Mwaka 2021 Membe aliripotiwa kuwa alijitahidi kurudi CCM. Kwenye Oktoba 2021 alishinda kesi yake ya mwaka 2018 dhidi ya Cyprian Musiba mhariri wa Tanzanite aliyehukumiwa kumlipa Membe TSh bilioni 6[5].
Tazama pia
Marejeo
- ↑ "Mengi kuhusu Bernard Kamilius Membe". 26 Juni 2008. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-19. Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2011.
- ↑ https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/huyu-ndiye-bernard-kamillius-membe-4232388
- ↑ [https://dailynews.co.tz/news/2019-12-145df464d1b16f1 CCM Bigwigs walking tightrope] Daily News 14.12.2019
- ↑ https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/bernard-membe-quits-act-wazalendo-3245458 Archived 29 Oktoba 2021 at the Wayback Machine. Benrand Membe quits ACT Wazalendo, Mwananchi ya 02.01.2021
- ↑ https://www.ippmedia.com/sw/habari/membe-kulipwa-fidia-ya-bilioni-6-na-musiba Membe kulipwa fidia ya bilioni 6 na Musiba, gazeti la Guardian tar. 20.10.2021
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |