Nenda kwa yaliyomo

Aurelius wa Karthago

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa Antonello wa Messina.

Aurelius wa Karthago (alifariki 429 hivi) alikuwa askofu wa Karthago (leo nchini Tunisia) kuanzia mwaka 391 hivi hadi kifo chake.

Nguzo imara ya Kanisa, alikinga waamini dhidi ya desturi za Kipagani akaweka kiti chake cha askofu mahali palipokuwa kwanza na sanamu ya mungu jike wa mbingu[1].

Aliendesha mitaguso mingi ya kutetea imani sahihi.

Augustino wa Hippo alimheshimu Aurelius, na barua kadhaa walizoandikiana zimetufikia. Ni kwamba Augustino alipokuwa padri huko Hippo na alitaka kuanzisha monasteri Aurelius alimsadia kupata pesa na watakaji, ambao hivyo waliweza kuandaliwa hata kuwa maaskofu baadaye.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Julai[2].

Masalia yake yanatunzwa Hirsau Abbey, huko Ujerumani.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Maandishi yake

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.