Atanasi Bazzekuketta
Atanasi Bazzekuketta (1866 - Nakivubo 27 Mei 1886) ni mfiadini mmojawapo kati ya Wakristo 22 wa Kanisa Katoliki wanaojulikana na kuheshimiwa duniani kote kama Wafiadini wa Uganda.
Hao walikuwa wahudumu wa ikulu ya kabaka wa Buganda Mwanga II (1884 - 1903) ambao waliuawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885 na tarehe 27 Januari 1887 kwa sababu ya kumwamini Yesu Kristo baada ya kuhubiriwa Injili na Wamisionari wa Afrika walioandaliwa na kardinali Charles Lavigerie.
Hawa ndio wafiadini wa kwanza wa Kusini kwa Sahara kuheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 3 Juni, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 27 Mei[1].
Siku hiyo, wakati wa kupelekwa kuuawa pamoja na wenzake, aliwaomba watesi wammalize haraka, nao wakampiga fimbo hadi kufa. Alikuwa amebatizwa tangu muda mfupi tu[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Mabradha wa Shule za Kikristo
- Orodha ya Watakatifu Waaugustino
- Orodha ya Watakatifu Wabazili
- Orodha ya Watakatifu Wabenedikto
- Orodha ya Watakatifu Wadominiko
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Watakatifu Wajesuiti
- Orodha ya Watakatifu Wakarmeli
- Orodha ya Watakatifu Wakolumbani
- Orodha ya Watakatifu Wamersedari
- Orodha ya Watakatifu Waoratori
- Orodha ya Watakatifu Wapasionisti
- Orodha ya Watakatifu Wapremontree
- Orodha ya Watakatifu Waredentori
- Orodha ya Watakatifu Wasalesiani
- Orodha ya Watakatifu Waskolopi
- Orodha ya Watakatifu Wateatini
- Orodha ya Watakatifu Watrinitari
- Orodha ya Watakatifu Watumishi wa Maria
- Orodha ya Watakatifu Wavinsenti
- Wafiadini wa Uganda
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- J. FRANSE, W.F., Mashahidi 22 wa Uganda – tafsiri ya C. Kuhenga n.k. – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1981
- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 190-194
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 160-162
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |