Andrea Hubati Fournet

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Andrea Hubati akisali.

Andrea Hubati Fournet (Saint-Pierre-de-Maillé, Vienne, 6 Desemba 1752La Puye, 13 Mei 1834) alikuwa padri mwanajimbo wa Kanisa Katoliki kutoka Ufaransa, ingawa hapo awali hakupenda dini.

Wakati wa Mapinduzi ya Kifaransa kwa miaka mingi alifanya kazi ya uchungaji kama paroko wa kijiji alimozaliwa, akiimarisha imani ya waumini [1].

Aliwahi kufungwa kwa kukataa kiapo haramu lakini alifaulu kutoroka akaishi Hispania miaka mitano.

Hatimaye, baada ya dhuluma hiyo kwisha, alianzisha shirika la Masista wa Msalaba pamoja na Yoana Elizabeti Bichier des Ages[2].

Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 16 Mei 1926, halafu kuwa mtakatifu tarehe 4 Juni 1933[1].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "San Andrea Hubert Fournet". Santi e Beati. Iliwekwa mnamo 11 November 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Saint André-Hubert Fournet". Saints SQPN. 6 August 2012. Iliwekwa mnamo 11 November 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.