Nenda kwa yaliyomo

Andrea Dung-Lac

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Andrew Dũng-Lạc, katika kioo cha rangi, St. Paul's R.C. Church, Westerville, Ohio, Marekani.

Andrea Dũng-Lạc (kwa Kivietnam: Anrê Trần An Dũng Lạc; 179521 Desemba 1839) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Vietnam hadi alipokatwa kichwa chini ya utawala wa Minh Mạng kwa sababu alikataa kukashfu msalaba wa Yesu [1].

Alitangazwa na Papa Leo XIII kuwa mwenye heri tarehe 24 Novemba 1900, halafu na Papa Yohane Paulo II kuwa mtakatifu mfiadini tarehe 19 Juni 1988.

Sikukuu yake huadhimishwa kila tarehe 24 Novemba[2] pamoja na kundi la wenzake 116 linalojumlisha Wafiadini wa Vietnam wa karne ya 17, 18 na 19 (dhuluma zilidumu miaka 16251886).

Trần An Dũng alizaliwa katika familia ya wakulima fukara sana, kiasi kwamba ilimuuza akiwa mtoto wa kambo kwa katekista Mkatoliki.

Huyo alimlea vizuri na kumsomesha. Wakati wa kubatizwa alichukua jina la Anrê (Andrea).

Alipata upadrisho tarehe 15 Machi 1823 akafanywa paroko.[3]

Wakati wa dhuluma ya kidini alitumia jina la Lạc ili kuendelea na utume wake,[4] lakini hatimaye alikamatwa na kufungwa.

Mara kadhaa alikombolewa na waumini wake kwa pesa akakamatwa tena sehemu nyingine.

Hatimaye aliuawa pamoja na padri aliyemkaribisha, Petro Trương Văn Thi [5].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/25400
  2. Martyrologium Romanum
  3. Michael Walsh, ed. "Butler's Lives of the Saints." HarperCollins Publishers: New York, 1991, p. 390.
  4. Phát Huồn Phan Việt-Nam giáo-sử - 1962 - Volume 2 - Page 73 "Vẩn đề trường Dũng-Lạc đã làm cho đư-luận công-giáo Hà-thành sôi nồi. Trường Dũng-lạc là một trường tư-thục công-giáo ớ sát cạnh nhà thờ lớn đo cha chính Nguyễn-vỉn-Vinh làm hiệu-trướng. Ðầu niên- khóa, học sinh xin vào học rết ..."
  5. https://www.santiebeati.it/dettaglio/97468

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.