Nenda kwa yaliyomo

Allen Johnson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rekodi za medali

Johnson katika mbio ya 2007 ISTAF Berlin
Riadha ya Wanaume
Anawakilisha nchi Marekani Marekani
Michezo ya Olimpiki
Dhahabu 1996 Atlanta 110 m urukaji viunzi
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya IAAF
Dhahabu 1995 Gothenburg 110 m urukaji viunzi
Dhahabu 1997 Athens 110 m urukaji viunzi
Dhahabu 2001 Edmonton 110 m urukaji viunzi
Dhahabu 2003 Paris 110 m urukaji viunzi
Medali ya Shaba 2005 Helsinki 110 m urukaji viunzi
Mashindano ya Mabingwa ya Ndani ya Ukumbi
Dhahabu 1995 Barcelona 60 m urukaji viunzi
Dhahabu 2003 Birmingham 60 m urukaji viunzi
Dhahabu 2004 Budapest 60 m urukaji viunzi
Fedha 2008 Valencia 60 m urukaji viunzi

Allen Kenneth Johnson (alizaliwa 1 Machi 1971) ni mwanariadha wa mbio za kuruka viunzi aliyeshinda medali ya dhahabu katika mbio ya 110m na urukaji viunzi katika michezo ya Olimpiki ya 1996,Atlanta,Georgia.

Aliyezaliwa mjini Washington D.C.,ni mwanamichezo bora na alisoma katika Chuo Kikuu cha Carolina Kaskazini alipofuzu katika michezo mbalimbali.

Johnson alipata majeraha katika mwaka wa 2000 lakini bado katika juhudi zake alifika fainali ya mbio yake katika Olimpiki ya 2000 huko Sydney,Australia.Alichukua nafasi ya nne katika fainali akishindwa na kidogo tu.

Mwaka wa 2003 katika Stade de France,Johnson alishinda medali yake ya nne ya dhahabu katika mbio za IAAF za Mabingwa wa Dunia katika 110m ya urukaji viunzi akishinda Terrence Trammell.Hii ilishinda medali tatu alizoshinda Greg Foster katika mashindano ya IAAF.

Katika Olimpiki ya 2004,alijikwaa na kiunzi katika awamu ya pili ya kuhitimu na hivyo basi akashindwa kumaliza mbio hiyo na hakufika fainali. Hata hivyo,aliorodheshwa kama nambari ya kwanza duniani katika msimu wa 2004.

Johnson hufanya mazoezi chini ya Kocha Curtis Frye katika Chuo Kikuu cha Carolina Kusini ambapo anafanya kazi kama kocha msaidizi wa kujitolea. Yeye anaishi Irmo,katika eneo la South Carolina.

Muda wake bora wa kibinafsi ni sekunde 12.92,imekosa kufikia rekodi ya Colin Jackson kwa sekunde 0.01 na sekunde 0.05 nyuma ya rekodi ya Dayron Robles. Johnson amemaliza mbio 11 halali kwa muda ulio chini ya sekunde 13,nyingi kuliko mtu mwingine hivi sasa.

Mafanikio

[hariri | hariri chanzo]

(Mbio ya mita 110 ya urukaji viunzi)

  • 1994
  • 1995
    • Mashindano ya Mabingwa wa Dunia katika Riadha ya 1995 - Gothenburg, Uswidi
      • Or Dhahabu
    • 1995 IAAF Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Ndani ya Ukumbi - Barcelona, Uhispania
      • Or 60 m Urukaji viunzi, Dhahabu
  • 1996
    • Olimpiki ya 1996 - Atlanta, Georgia
      • Or Dhahabu, Rekodi ya Olimpiki
    • Mashindano ya Mabingwa wa Dunia katika Riadha ya 1997 - Athens, Ugiriki
      • Or Dhahabu
  • 1998
  • 2000
  • 2001
  • 2002
    • Mashindano ya Kombe la Dunia ya 2002 - Madrid, Uhispania
      • Argent Fedha
  • 2003
    • Mashindano ya Mabingwa wa Dunia katika Riadha ya 2003 - Paris, Ufaransa
      • Or Dhahabu
    • Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya IAAF ya Ndani ya Ukumbi ya 2003 - Birmingham, Uingereza
      • Or 60 m Urukaji viunzi, Dhahabu
  • 2004
    • Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya IAAF ya Ndani ya Ukumbi ya 2004 - Budapest, Hungaria
      • Or 60 m Urukaji viunzi, Dhahabu
  • 2005
    • Mashindano ya Mabingwa wa Dunia katika Riadha ya 2005 - Helsinki, Finland
      • Bronze Shaba
  1. Orodha ya IAAF ya wanariadha bora katika 110m

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]



Alitanguliwa na
Colin Jackson
Wanaume Bora katika mbio ya 110m ya urukaji viunzi wa Mwaka
1995 — 1998
Akafuatiwa na
Mark Crear
Alitanguliwa na
Mark Crear
Wanaume Bora katika mbio ya 110m ya urukaji viunzi wa Mwaka
2000 — 2001
Akafuatiwa na
Anier García
Alitanguliwa na
Anier García
Wanaume Bora katika mbio ya 110m ya urukaji viunzi wa Mwaka
2003
Akafuatiwa na
Liu Xiang