Nenda kwa yaliyomo

Jerboa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Allactaginae)
Jerboa
Jerboa mdogo (Jaculus jaculus)
Jerboa mdogo (Jaculus jaculus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Dipodidae (Wanyama walio na mnasaba na mabuku)
Fischer von Waldheim, 1817
Ngazi za chini

Nusufamilia 4 (spishi 4 katika Afrika):

Jerboa ni wanyama wagugunaji wa nusufamilia Allactaginae, Cardiocraniinae, Dipodinae na Euchoreutinae katika familia Dipodidae wanaofanana na kanguruu wadogo kwa sababu wana miguu mirefu ya nyuma na miguu mifupi ya mbele. Wanatokea maeneo makavu katika Afrika ya Kaskazini na Asia.

Jerboa ni wagugunaji wadogo hadi wa kadiri wenye urefu wa mwili wa sm 4-26 bila mkia, ambao ni mpaka maradufu wa urefu wa mwili. Wote wametoholewa kwa kuruka ingawa kwa viwango tofauti. Wana miguu mirefu sana ya nyuma ambayo, katika spishi nyingi, inajumuisha mifupa mirefu ya metakarpali. Wanasonga ama kwa kuruka au kwa kutembea kwa miguu yao ya nyuma. Mkia mrefu wa jerboa husaidia katika kuweka usawaziko wao.

Wengi ni walavyote na lishe yao ni mbegu na wadudu. Spishi kadhaa za jerboa hata hivyo, kama Allactaga sibirica, ni karibu walawadudu kabisa. Kama wagugunaji wengine wana meno ya mbele ya kutafuna yaliyotengwa kwa pengo (diastema) na meno ya shavu ya kusaga.

Jerboa hufanya viota vyao kwenye vishimo ambavyo vinaweza kuwa tata kwa vyumba vya pembeni ambapo huhifadhi chakula chao. Spishi nyingi hulala wakati wa baridi kwa angalau nusu mwaka zikinusurika kwa mafuta zinayounda katika wiki kadhaa kabla ya kulala.

Majike huzaa wachanga wawili hadi saba baada ya kipindi cha ujauzito kati ya siku 17 na 42. Wanazaana mara moja au mbili kwa mwaka kulingana na spishi.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Asia

[hariri | hariri chanzo]