Albin Ekdal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Albin Ekdal
binadamu
Jinsiamume Hariri
Nchi ya uraiaUswidi Hariri
Nchi anayoitumikiaUswidi Hariri
Jina halisiAlbin Hariri
Jina la familiaEkdal Hariri
Tarehe ya kuzaliwa28 Julai 1989 Hariri
Mahali alipozaliwaStockholm Hariri
BabaLennart Ekdal Hariri
NduguHjalmar Ekdal Hariri
Kaziassociation football player Hariri
Nafasi anayocheza kwenye timuKiungo Hariri
Muda wa kazi2007 Hariri
Medical conditionCOVID-19 Hariri
MchezoMpira wa miguu Hariri
Namba ya Mchezaji8 Hariri
AmeshirikiKombe la Dunia la FIFA 2018, UEFA Euro 2016 Hariri
LigiBundesliga Hariri

Albin Ekdal (alizaliwa 28 Julai 1989) ni mshambuliaji wa Uswidi ambaye anacheza kama kiungo wa klabu ya Sampdoria iliyopo Serie A ya Italia.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Brommapojkarna[hariri | hariri chanzo]

Albin Ekdal alianza kazi yake ya kucheza akiwa na klabu ya Brommapojkarna mwanzoni mwa msimu wa 2007 Allsvenskan. Alicheza hasa kama kiungo mkabaji lakini pia kama kiungo mshambuliaji.

Juventus[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 23 Mei 2008, alisaini mkataba wa miaka minne na klabu Juventus F.C .. Ekdal alikata kusaini katika klabu nyingine, ikiwa ni pamoja na Chelsea na Inter, kabla ya kusaini makataba na klabu ya Juventus FC. Ekdal alicheza Serie A kwa maraya kwanza mnamo 18 Oktoba 2008 katika mechi ambayo walifungwa 1-2 dhidi ya klabu ya Napoli wakati aliingia kama mchezaji wa akiba dakika ya 75, akichukua nafasi ya Christian Poulsen.

Siena[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 15 Julai 2009, A.C. Siena walimsaini Ekdal kwa mkopo kutoka katika klabu ya Juventus F.C. alcheza mechi 27.

Bologna[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 28 Juni 2010, Juventus F.C. waliuza 50% ya hisa zao Ekdal katika klabu ya Bologna.

Cagliari Calcio[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 21 Agosti 2011 aliuzwa katika mpango wa ushirikiano na klabu ya Serie A wenzake Cagliari Calcio. Mnamo tarehe 28 Septemba 2014, Ekdal alifunga goli lake la kwzanza katika klabu ya Cagliari baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Inter Milan.

Hamburger SV[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 18 Julai 2015,alisajiliwa katika klabu ya Ujerumani itwayo Hamburger SV alisaini kutoka katika klabu ya Cagliari kwenye mpango wa miaka minne(4) kwa pauni 4.5 milioni a.Alipewa jezi ya namba 20. Tarehe 3 Machi 2017, Ekdal alifunga goli lake la kwanza katika ligi ya Bundesliga katika ushindi wa 1-0 dhidi ya klabu yaHertha BSC.

Sampdoria[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 14 Agosti 2018, baada ya miaka mitatu (3) akiwa na klabu ya Hamburger SV, Ekdal alirudi tena Serie A kwa kusaini mkataba katika klabu ya Sampdoria.

Kazi ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Ekdal alicheza kwa mara ya kwanza katika Timu ya taifa ya Uswidi mnamo 10 Agosti 2011 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ukraine.Mnamo Mei 2018 alitajwa katika kikosi cha watu 23 kwa ajili ya kuiwakilisha nchi ya Uswidi katika Kombe la Dunia la FIFA 2018 nchini Urusi.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Albin Ekdal kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.