Nenda kwa yaliyomo

Agnes wa Roma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nakshi za mawe za Agnes Mtakatifu katika kanisa la "Santa Agnese fuori le mura" huko Roma.

Agnes wa Roma (alifariki mjini Roma, Italia, 304) alikuwa bikira mwenye umri wa miaka 12 aliyekataa kuolewa kutokana na imani yake ya Kikristo.

Kwa sababu hiyo aliteswa akauawa wakati wa dhuluma ya Dola la Roma dhidi ya Wakristo.

Habari zake hazieleweki waziwazi kama aliishi wakati wa Kaisari Decius au wakati wa Kaisari Diokletian ambao wote wawili waliamuru mateso ya Wakristo, lakini mwelekeo wa wanahistoria ni kukubali jibu hilo la pili.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 21 Januari[1].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikisource ina maelezo kamili yahusianayo na makala hii:
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.