Agabo
Jump to navigation
Jump to search
Agabo (kwa Kigiriki Ἄγαβος, Agabos) alikuwa mmojawapo kati ya Wakristo wa kwanza kati ya Palestina na Siria.
Anatajwa mara mbili na kitabu cha Matendo ya Mitume kama nabii.
Agabo anaheshimiwa kama mtakatifu na madhehebu mbalimbali ya Ukristo.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Februari au 8 Machi.
Habari zake[hariri | hariri chanzo]
Kadiri ya Mdo 11:27-28, alikuwa mmoja wa manabii waliofika Antiokia kutoka Yerusalemu na alitabiri njaa kali iliyotokea wakati wa kaisari Klaudio.
Kadiri ya Mdo 21:10-12, miaka mingi baadaye 58 hivi, Agabo alikutana na Mtume Paulo huko Kaisarea Maritima akamtabiria atakavyokamatwa hivi karibuni.
Kadiri ya mapokeo alikuwa mmojawapo kati ya wanafunzi 70/72 wa Yesu na alifia dini huko Antiokia.
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- "Agabus" at the Catholic Encyclopedia. Retrieved January 10, 2006.