Nenda kwa yaliyomo

Abderrahmane Abdelli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Abderrahmane
Kazi yake Mwanamuziki


Abderrahmane Abdelli akicheza mandol (mandole ya Algeria) katika tamasha huko Ghent, Ubelgiji mnamo Oktoba 1, 2006

Abderrahmane Abdelli (alizaliwa Aprili 2, 1958), ni mwandishi wa Kiberber na mtunzi wa nyimbo anayejulikana kwa kuchanganya muziki wa kitamaduni wa huko Afrika ya Kaskazini kwa upigaji wa gitaa.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Abdelli nimzaliwa wa Mechta Behalil Algeria, wakati wa vita vya Uhuru wa Algeria. Familia yake ilihamishwa na mlipuko katika kijiji chao, Kennour, [1] sehemu ya Mkoa wa Tizi Ouzou, na jeshi la anga la Ufaransa. Baada ya vita, familia ya Abdelli ilikaa katika mji wa pwani wa Dellys . Akiwa mvulana, Abdelli alitengeneza gitaa lake la kwanza kutoka kutokana na kopo tupu la mafuta, ubao wa mbao na kamba ya uvuvi. [2] Baada ya kujifunza kupiga gitaa, Abdelli alitambulishwa kwa mandol na bwana Chaabi, Chaïd Moh-Esguir. [2]

Abdelli alianza muziki wake kwa mara ya kwanza huko Dellys, Kabylie, wakati wa tamasha la Uhuru wa Algeria mwaka 1974. [3] Alishinda mashindano kadhaa nchini Algeria kwa waimbaji mahiri. [4] Abdelli alitoa albamu yake ya kwanza mnamo 1984, lakini haikufanikiwa. Miaka miwili baadae, alitoa albamu ambayo iliuza nakala 12,000, lakini hakuwahi kupokea malipo kutoka katika kampuni yake ya rekodi ya Abdelli ilitoa albamu kadhaa nchini Algeria, lakini alihamia Ubelgiji mwaka 1984.. Ndipo alipokutana na mtayarishaji Thierry Van Roy, ambaye alivutiwa sana na muziki wa Abdelli hivi kwamba alitumia miaka miwili kuchunguza mizizi ya mapokeo ya muziki ya Waberber katika Chuo Kikuu cha Algiers." [4] Tangu 1986 amejenga makazi yake huko Brussels, Ubelgiji.

Albamu maarufu zaidi za Abdelli ni pamoja na New Moon [5] na Among Brothers [6] Ametumbuiza kwenye matamasha mbalimbali barani Ulaya, ikiwa ni pamoja na WOMAD na tamasha la 0110 concert huko Ghent . Mbali na Ulaya ametembelea Uingereza, Marekani na Kanada.

Orodha ya kazi zake za kimuziki (Diskografia)[hariri | hariri chanzo]

 • New Moon (1995)
 • Au-delà de Gibraltar (2000)
 • Among Brothers (2003)
 • Destiny (2011)

Washiriki katika bendi[hariri | hariri chanzo]

 • Roberto Lagos (charango, guitar, bombo)
 • Said Mohammed (ney)
 • Jazouli Azzedine (darbuka, tar, bendir)
 • Louis Ivan Leiva Alguinta ((Latin percussion)
 • Abdelmajid Makrai Lamarti (violin)
 • Thierry Van Roy (keyboards)


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Locator Map for Kennour, Algeria from Nona.net
 2. 2.0 2.1 "Biography: Abdelli" GekkoBeat.com
 3. ""Abdelli Biography" Thierry Van Roy Productions". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Septemba 16, 2018. Iliwekwa mnamo Novemba 8, 2006.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 4. 4.0 4.1 ""Abdelli" World Music Central". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 17, 2011. Iliwekwa mnamo Novemba 8, 2006.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 5. Abdelli (1995) New Moon Real World, New York, CDRW54, arranged by Thierry Van Roy, recorded by Thierry Van Roy Studios, Brussels, Belgium;
 6. Abdelli (2003) Among Brothers Real World Records, Virgin Music, Wiltshire, UK, arranged by Thierry Van Roy, recorded in various locations between Nov. 1998 and May 2001;
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Abderrahmane Abdelli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.