Mbuga za Taifa la Tanzania
Mbuga za Taifa za Tanzania[1] ni nyingi tena mbalimbali, zikishika karibu theluthi moja ya eneo lote la nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Zinagawanyika kati ya:
- Hifadhi za Taifa,
- Hifadhi Teule,
- Hifadhi ya Mawindo na
- Mapori ya Akiba.
Hifadhi za taifa
[hariri | hariri chanzo]Hii ni orodha ya Hifadhi za Taifa, ambazo ni 19:
Hifadhi za Taifa | Kiingereza | Mkoa |
---|---|---|
Hifadhi ya Arusha | Arusha NP | Arusha |
Hifadhi ya Burigi-Chato | Burigi-Chato NP | Kagera, Geita |
Hifadhi ya Gombe | Gombe Stream NP | Kigoma |
Hifadhi ya Ibanda-Kyerwa | Ibanda-Kyerwa NP | Kagera |
Hifadhi ya Katavi | Katavi NP | Simiyu |
Hifadhi ya kisiwa cha Rubondo | Rubondo Island NP | Mwanza |
Hifadhi ya kisiwa cha Saanane | Saanane Island NP | Mwanza |
Hifadhi ya Kitulo | Kitulo Plateau NP | Njombe |
Hifadhi ya Mikumi | Mikumi NP | Morogoro |
Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro | Mount Kilimanjaro NP | Kilimanjaro |
Hifadhi ya Milima ya Mahale | Mahale Mountains NP | Kigoma |
Hifadhi ya Milima ya Udzungwa | Udzungwa Mountains NP | Iringa, Morogoro |
Hifadhi ya Mkomazi | Mkomazi NP | Kilimanjaro, Tanga |
Hifadhi ya Ruaha | Ruaha NP | Iringa |
Hifadhi ya Rumanyika-Karagwe | Rumanyika-Karagwe NP | Kagera |
Hifadhi ya Saadani | Saadani NP | Pwani |
Hifadhi ya Serengeti | Serengeti NP | Mara |
Hifadhi ya Tarangire | Tarangire NP | Manyara |
Hifadhi ya Ziwa Manyara | Lake Manyara NP | Manyara |
Hakuna budi kuweka ulinzi mbugani kwani kuna majangili wanaoua ovyo wanyama kama vile tembo na kifaru: wanyama hao wanaweza kusaidia katika kuinua pato la taifa kupitia utalii.
Hifadhi za bahari na maeneo tengefu
[hariri | hariri chanzo]Ni mpango wa kimataifa kuwa asilimia 10 ya maji ya bahari na maziwa yawe chini ya hifadhi, na Tanzania ina asilimia 4.5 tu ya hifadhi ambayo inahusisha hifadhi za bahari 3 na maeneo tengefu 15.
Hifadhi za bahari
[hariri | hariri chanzo]Hifadhi ya Bahari ni eneo kubwa ambalo hata watu wanaishi ndani yake. Shughuli za eneo hilo husimamiwa na Mpango wa Usimamiaji ujulikanao kama General Management Plan, ambao maandalizi yake yanashirikisha wadau woteː wanaoishi ndani ya hifadhi, Halmashauri husika ambazo ziko ndani ya hifadhi, na wengineo wakiwa ni pamoja na wanasayansi. Yanafanyika makubaliano ya kuwa baadhi ya maeneo yatengwe kabisa ambapo hakuna uvuvi wowote utakaoruhusiwa, kutenga maeneo ya matumizi ya jumla ambapo uvuvi unaruhusiwa kwa wavuvi wa ndani na nje ya hifadhi na maeneo ya matumizi maalum ambayo pamoja na kwamba wavuvi wa ndani ya hifadhi wanaruhusiwa kuvua kwa kutumia zana maalumu zinazokubalika, wavuvi wa nje hawaruhusiwi kabisa kuvua katika maeneo hayo.
Maeneo tengefu
[hariri | hariri chanzo]Maeneo tengefu ni maeneo madogomadogo ya visiwa ambayo yanazungukwa na matumbawe. Katika maeneo hayo watu hawaruhusiwi kuishi wala matumizi ya rasilimali hayaruhusiwi. Shughuli zinazoruhusiwa katika maeneo hayo ni zile zinazohusiana na utalii tu. Maeneo hayo ni pamoja na visiwa vya Bongoyo na Mbudya mjini Dar es Salaam ambapo ndani yake kitengo kimetengeneza njia vinjari (nature trails) kwa ajili ya watalii kupita.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ ["TANAPA, Tanapa Brocha (Kiingereza)" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2012-09-20. Iliwekwa mnamo 2009-08-10. TANAPA, Tanapa Brocha (Kiingereza)]
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi ya Mbuga za Taifa za Tanzania
- UNEP WCMC Archived 11 Juni 2007 at the Wayback Machine.
- Marine Parks in Tanzania Archived 15 Mei 2010 at the Wayback Machine.
- Morogoro Conservation Area Authority (Kiingereza)