Hifadhi ya Mikumi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hifadhi ya Mikumi: lango la kuingilia.
Twiga ndani ya Hifadhi ya Mikumi.

Hifadhi ya Mikumi ni moja kati ya hifadhi za Taifa[1] mashuhuri na kubwa nchini Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 3230, hivyo inashika nafasi ya nne nchini[2].

Inapatikana katika Mkoa wa Morogoro na ilianzishwa mwaka wa 1964.

Ipo umbali wa kilometa 283 magharibi kwa Dar es Salaam. Aidha hifadhi hii iko kaskazini kwa mbuga ya Selous (Game Reserve) na iko barabarani unapoelekea katika hifadhi ya Udzungwa, mbuga ya wanyama ya Selous na Ruaha kwa barabara kutoka Dar es Salaam. Inapakana pia na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Uluguru.

Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapatikana ndani ya hifadhi hii.

Mbuga za wazi ndizo zinazoshamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.

Ndani ya hifadhi ya Mikumi kuna simba ambao huwa wanaonekana wakiwa katika himaya yao na mara nyingine wakiwa juu ya matawi ya miti ili kukwepa majimaji wakati mvua zinapototesha ardhi ambayo ina udongo wa mfinyanzi.

Makundi makubwa ya viboko, pundamilia na nyumbu huonekana katika eneo hili.

Wanyama wengine wengi hukimbilia katika eneo la miombo nyakati za mvua ambako unaweza kuwaona katika safu za milima. Hapo makundi makubwa ya nyati katika ukanda wa miombo wanaweza kuonekana.

Kwa upande wa ndege, wakati wa mvua huongezeka na kufikia zaidi ya aina 300. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, nyakati hizi kunakuwa na makundi ya ndege wahamiaji kutoka nchi za Ulaya na Asia ambayo huungana na makundi ya ndege wakazi kama vile chole.

Tunashauriwa kuwalinda wanyama ili watusaidie kuongeza pato kupitia sekta ya utalii.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-11-14. Iliwekwa mnamo 2020-08-18.
  2. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-11-13. Iliwekwa mnamo 2020-08-18.

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Mikumi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.