Martin de Porres
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Martin de Porres (1579 – 3 Novemba 1639) alikuwa bradha wa Shirika la Wahubiri katika nchi ya Peru.
Akiwa mtoto chotara wa mkabaila Mhispania Juan de Porres na binti mwenye asili ya Afrika Anna Velasquez hakutambuliwa na baba yake akalelewa na mama na kuwa msaidizi wa daktari akijifunza hivyo elimu ya matibabu.
Mwaka 1594 alijiunga na watawa Wadominiko akaendelea kuwaangalia wagonjwa wa tabaka na rangi zote.
Kutokana na upendo aliowaonyesha watu wote aliheshimiwa sana na taarifa za uponyaji wa ajabu zilianza kuenea.
Mwaka 1837 alitangazwa mwenye heri na Papa Gregori XVI, halafu tarehe 6 Mei 1962 akatangazwa na Papa Yohane XXIII kuwa mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 3 Novemba.
Marejeo [hariri]
- BENEDICTINE FATHERS – Rafiki Martin, Habari za Maisha ya Mtakatifu Martin De Porres O.P. – Kipigo Chapa cha Tano ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1990 – ISBN 9976-63-057-3
Viungo vya nje [hariri]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- St. Martin de Porres website and image
- Saint of the Day, November 3: Martin de Porres
- Prayer for the intercession of St. Martin de Porres
- Order of Preachers: Southern Dominican Province of St. Martin de Porres
- St. Martin de Porres Shrine & Institute • Memphis, Tennessee
- St. Martin De Porres, First Black Saint Of The Americas, Celebrated Nov. 3
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Martin de Porres kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |