Bradha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bradha Mfransisko

Bradha au bruda ni namna ya kutaja watawa wanaume Wakristo wasio makasisi. Maneno haya yamepokelewa katika Kiswahili kutoka Kiingereza "brother" au Kijerumani "Bruder".

Hali ya kuwekwa wakfu kwa kuahidi utekelezaji wa mashauri ya Kiinjili (useja mtakatifu, ufukara, utiifu)) inajitosheleza kama ilivyo kwa masista. Kwa kuwa lengo la utawa si kuongoza Kanisa kwa mamlaka inayotokana na daraja takatifu au kutoa huduma za kipadri, bali ni kulenga utakatifu, yaani upendo kamili.