Karne ya 1
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Karne I)
Lango la Historia | Lango la Biografia | Karibuni | Orodha ya Miaka
◄ | Karne ya 2 KK | Karne ya 1 KK | Karne ya 1 | Karne ya 2 | Karne ya 3 | ►
Miaka ya 0 | Miaka ya 10 | Miaka ya 20 | Miaka ya 30 | Miaka ya 40 | Miaka ya 50 | Miaka ya 60 | Miaka ya 70 | Miaka ya 80 | Miaka ya 90
Karne ya 1 ilikuwa kipindi cha miaka mia moja kati ya 1 na 100. Kikamilifu kilianza tarehe 1 Januari 1 B.K. na kuishia 31 Desemba 100. Namba zake zinafuata hesabu ya miaka "baada ya Kristo".
Kama kila "karne" ni kipindi kinachohesabiwa kwa hiari ya kibinadamu kwa sababu ni mgawanyo wa kalenda tu: katika hali halisi maendeleo na mabadiliko makubwa hayafuati migawanyo ya kalenda ya kibinadamu.
Kuna mambo mengi yaliyotokea wakati wa karne hii.
Karne ya Ukristo kuanza [hariri]
- Yesu Kristo, akitanguliwa na Yohane Mbatizaji, anahubiri na kuuawa katika nchi ya Palestina
- Dini mpya ya Ukristo inaanza na kuenea haraka hadi Ulaya magharibi na labda India kusini
- Vitabu vya Agano Jipya vinaandikwa
- Dola la Roma linafurahia amani iliyopatikana kuanzia utawala wa Kaisari Augusto
- Maangamizi ya Yerusalemu na hekalu lake