Zuhura Yunus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Zuhura Yunus (amezaliwa tar.) ni mtangazaji wa BBC, idhaa ya Kiswahili ambaye amekuwa mwanamke wa kwanza kutangaza kipindi cha Dira ya Dunia.[1]

Maisha na kazi[hariri | hariri chanzo]

Licha ya kuwa mtangazaji Zuhura Yunus alikuwa na ndoto ya kuwa daktari, lakini aliachana na ndoto yake hiyo na kujiunga na utangazaji wa redioni mwaka 2000 nchini Tanzania.

Kabla ya kujiunga na BBC alifanya kazi ya utanzangaji katika vipindi mbalimbali vya redio kama Redio Times FM na Uhuru FM nchini Tanzania.

Mwaka 2002 alifanya kazi ya uandishi wa habari katika gazeti la The Citizen. Mwaka 2008 aljiunga na BBC Swahili akiwa mtangazaji na mtayarishaji wa matangazo.

Zuhura ameripoti na kutangaza uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2010, Mbio za Marathon za London na habari nyingine mbalimbali kwenye redio ya BBC.

Tuzo mbalimbali[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2000 alishinda tuzo ya habari ya Ishi nchini Tanzania kutokana na ripoti yake kuhusu virusi vya ukimwi na Ukimwi[2].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zuhura Yunus kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.