Nenda kwa yaliyomo

Ziji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ziji ya Timbuktu
Ziji ya Khwarizmi

Ziji (kutoka Kiajemi: زيج, zīj) katika elimuanga ni kitabu chenye majedwali yatoayo mwendo wa gimba la angani (hasa nyota au sayari); yaani mahali na kasimwelekeo yake katika muda fulani.[1] Ziji zikiwa muhimu sana kwa usafiri baharini, kuzikokotoa kulikuwa mojawapo kati ya matumizi ya kwanza ya tarakilishi za mitambo. Siku hizi, ziji hutolewa kielektroniki na hutumika kwa usafiri wa anga-nje.

Ziji ya kisasa[hariri | hariri chanzo]

Ziji ya kisasa, badala ya kitabu kama zile za zamani, ni maunzilaini yaletayo mahali pa sayari, miezi, visayari, au nyotamkia, wakati wowote unaotakiwa na mtumiaji.

Baada ya kuanzishwa kwa tarakilishi za umeme miaka ya 1950, ikawezekana kutumia ukamilishaji wa namba ili kuhesabu ziji. Mfano bora ni Ziji ya Maendeleo ya Maabara ya Nguvu wa Jeti. Ziji zilizo sahihi kuliko zile za zamani zimeendelezwa, zinazojulikana kama ziji changanuzi ambazo hutumia upanuzi wa mfululizo ili kukokotoa majiranukta na njia. Hiyo imeanza kuwezekana kwa sababu ya ubuni wa tarakilishi ziwezazo kuhesabu makumielfu ya vipengele katika upanuzi. Ephemeride Lunaire Parisienne na VSOP ni mifano.[2]

Ziji za Mfumo wa Jua ni muhimu kwa uongozaji wa vyombo vya angani na kwa aina mbalimbali za uchunguzi wa sayari, miezi, nyota, na majarra.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Knappert, Jan; van Kessel, Leo (2010). Wijsen, Frans; Tullemans, Harrie (whr.). Dictionary of Literary Swahili. uk. 671. ISBN 978-0-7734-3768-5.
  2. Simon, J. -L.; Francou, G.; Fienga, A.; Manche, H. (2013). "New analytical planetary theories VSOP2013 and TOP2013". Astronomy and Astrophysics (kwa Kiingereza). 557: A49. doi:10.1051/0004-6361/201321843. ISSN 0004-6361.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ziji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.