Kikokotozi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kikokotozi cha kibiashara.
Kikokotozi cha kisayansi.

Kikokotozi ni mashine ndogo ya hesabu inayotumika kukokotoa mambo mbalimbali yanayohusu hesabu.

Mashine hizi zipo za aina nyingi: katika hizi kuna zinazoweza kukokotoa hesabu za kawaida ambazo mara nyingi hutumika madukani na kwenye biashara nyinginezo na kuna zinazoweza kukokotoa hesabu za fizikia, kemia na hesabu ngumu ambazo haziwezi kufanywa na kikokotozi cha kawaida.

Mara nyingi hizi hutumiwa na wanahisabati na wanasayansi ili kufanya hesabu kwa wepesi na haraka.

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.