Khwarizmi
Muhammad ibn Mūsā al-Khwārizmī | |
---|---|
| |
Alizaliwa | mnamo 780 BK |
Alikufa | mnamo 850 |
Nchi | Dola la Waabasiya |
Kazi yake | mtaalamu wa hisabati, jiografia na falaki |
Muhammad ibn Musa al-Khwarizmi (Kiarabu: محمد بن موسى الخوارزمي) alikuwa mtaalamu wa hisabati, jiografia na falaki katika dola la Waabasiya aliyeishi muda mrefu mjini Baghdad.
Alizaliwa katika familia ya Kiajemi yenye asili katika kwenye milki ya Khwarezm. Haijulikana kama yeye mwenyewe alizaliwa huko. Hakuna habari alisoma wapi.
Khwarezmi alifanya kazi kwa muda mrefu katika Dar-al-Hikma (nyumba ya hekima) iliyokuwa kama chuo kikuu kilichoundwa na khalifa Harun ar-Rashid.
Katika kitabu chake juu ya "Mahesabu kwa kutumia namba za Kihindi" alionyesha faida ya hisabati ya Kihindi akaeleza namba sifuri. Hivyo aliweka msingi wa hisabati ya kisasa. Vitabu vyake vilitafsiriwa katika lugha mbalimbali vikasambazwa kwa Kilatini pia katika Ulaya.

Aliandika pia juu ya jiografia ya Ptolemayo akashiriki katika uchoraji wa ramani ya dunia kwa matumizi ya khalifa.
Utaalamu wake kuhusu falaki alitumia kwa vitabu vyake juu ya kalenda.