Zadar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Zadar
Kitovu cha mji wa Zadar
Kitovu cha mji wa Zadar

Bendera

Nembo
Nchi Kroatia
Wilaya
Idadi ya wakazi
 - 76,718

Zadar ni mji nchini Kroatia. Idadi ya wakazi wake ni takriban 76,718.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ni mji wa kihistoria uliojengwa kwenye nusukisiwa kando la Bahari ya Adria (Mediteranea). Zamani za Dola la Roma ilikuwa mji mkuu wa Dalmatia. Tangu mwaka 1000 mji ulijiunga na himaya ya Venezia lakini uatawala juu ya mji ulibadilika mara kwa mara kati ya jamhuri ya Venezia na wafalme wa Kroatia na Hungaria. Mwaka 1202 Zadar ilivamiwa na jeshi la vita ya misalaba ya 4 kwa niaba ya Venezia iliyotoa meli zake kwa kusafirisha jehi hili kwenda mashariki.

Mwaka 1409 mfalme wa Hungaria aliuza Dalmatia pamoja na Zadar kwa Venezia na hadi 1797 mji ulikuwa mji mkuu wa Dalmatia ya Kivenezia. Baada ya mwisho wa uhuru wa Venezia Zadar ilipitishwa chini ya mamlaka ya Austria ikabaki vile hadi 1918. Wakati ule wakazi wa Zadar walikuwa mchanganyiko wa watu waliosema Kiitalia na Kikroatia. Baada ya mwisho wa Austria-Hungaria eneo la Zadar lilikuwa sehemu ya Italia kutokana na asilimia kubwa ya wasemaji wa Kiitalia.

Mwisho wa vita kuu ya pili ya dunia wanamigambo wa kiongozi mkomunisti wa Yugoslavia Josip Broz Tito walivamia Zadar wakaua Waitalia na wengine walifukuzwa. Katika mkataba wa amani wa 1948 Italia ilikubali kukabidhi eneo la Zadar kwa Yugoslavia lilipokuwa sehemu ya jamhuri ya Kroatia ndani ya Yugoslavia.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Flag map of Croatia.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Kroatia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Zadar kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.