Yakutia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sehemu ya mkoa wa Yakutia
Mahali pa Yakutia Russia

Jamhuri ya Sakha (Yakutia) (kwa Kirusi: Республика Саха (Якутия)) ni jina la mkoa ulioko nchini Russia, katika sehemu yake ya Asia inayoitwa Siberia.

Mji mkuu ni Yakutsk.

Yakutia ina eneo la km² 3.083.523 (mara tatu eneo la Tanzania) lakini idadi ya wakazi ni 958.528 pekee (sensa ya 2010).

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Wakazi asilia ni Wasakha wanaoitwa pia Wayakuti. Lugha yao ni aina ya Kituruki. Siku hizi hao ni nusu ya wakazi wote, na Warusi ni karibu asilimia 38.

Wayakuti walikuwa kimapokeo wawindaji na wavuvi; kwenye kusini walifuga pia farasi na kulungu aktiki. Siku hizi wengi huishi mjini na kwenye vituo vya migodi ya madini mbalimbali.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Tabianchi kwenye kaskazini ya Siberia ni baridi sana. Sehemu kubwa ya Yakutia ni tundra; ardhi kwenye asilimia 40 za maeneo yake huganda daima ikitunza jalidi ya kudumu. Halijoto ya ardhi chini ya kina cha sentimita 30-200 haipandi juu ya sentigredi 0°C muda wote; hata wakati wa "joto" ni sentimita za juu pekee ambako barafu inayeyuka. Kwenye ardhi ya aina hii hakuna miti. Uoto wote katika sehemu hizi ni manyasi, kuvumwani na kuvu.

Kanda ya kusini, ambako jalidi ya kudumu inakwisha, kuna pia misitu ya taiga.

Upande wa kaskazini Yakutia, kama Siberia yote, inapakana na Bahari ya Aktiki.

Mito[hariri | hariri chanzo]

Mto Ura
Mto Olyokma

Sehemu kubwa ya jamhuri hii ni beseni la mto Lena lenye eneo la km² 4,400. Mto huo napokea mamia ya matawimto madogo. Mito mingine mikubwa ni pamoja na (kwa mabano urefu wa njia yake)

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Yakutia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.