Kaliningrad Oblast

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sehemu ya mkoa wa Kaliningrad Oblast
Mahali pa Kaliningrad Oblast katika Russia

Kaliningrad Oblast (rus. Калининградская область kalinin-grads-kaya oblast) ni jina la kutaja mkoa wa Urusi. Mji mkuu wake ni Kaliningrad (hadi 1945 Königsberg).

Eneo la Kaliningrad Oblast liko nje ya Urusi penyewe kati ya Poland na Lithuania.

Hadi mwaka 1945 ilikuwa sehemu ya jimbo la Prussia Mashariki katika Ujerumani. Kwenye mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia lilivamiwa na jeshi la Umoja wa Kisovyeti, wakazi Wajerumani walikimbia au walifukuzwa na mwaka 1946 eneo hili liliingizwa katika Jamhuri ya Kisovyieti ya Kirusi. Hata baada ya kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti mnamo mwaka 1991 eneno lilibaki sehemu ya Urusi.

Kisiasa eneo lina umuhimu mkubwa kutokana na bandari yake ya jeshi la majini wa Urusi na vituo vya roketi za kijeshi.

Kiuchumi wakazi wengi wanaona matatizo hasa kutokana na hali ya Kaliningrad ya kuwa mbali na taifa mama ikiviringishwa pande zote na nchi ambazo ni wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Kuna wakazi wapatao 942,000 (2010) na eneo lake ni km² 15,125.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kaliningrad Oblast kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.