Nenda kwa yaliyomo

Kirusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Rus.)

Kuhusu matumizi ya jina hili kwa viini vidogo vinavyosababisha magonjwa tazama Virusi

Nchi zenye wasemaji wa Kirusi (buluu: Kirusi kama lugha rasmi; kijani: Kirusi kama lugha mojawapo ya wakazi wa nchi)

Kirusi (русский язык russkiy yazik) ni moja kati ya lugha za Kislavoni cha Mashariki, ile yenye wasemaji wengi kati ya lugha zote za Kislavoni. Kirusi huandikwa kwa alfabeti ya Kisirili.

Kirusi ni lugha rasmi katika Urusi na pia katika nchi jirani za Belarus, Kazakhstan na Kirgizia. Wasemaji wa Kirusi wako katika nchi zote zilizokuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti hadi mwaka 1991. Kuna pia Warusi katika nchi za magharibi kwa sababu wakati wa Ukomunisti kulikuwa na wakimbizi waliotoka nje ya Urusi kwa sababu za kisiasa.

Pia watu wengi duniani wamejifunza Kirusi kwa sababu ilikuwa lugha ya kimataifa kati ya nchi zilizoshikamana na Umoja wa Kisovyeti. Wanafunzi wengi kutoka nchi mbalimbali za Afrika walipata elimu ya juu kwenye vyuo vikuu vya Umoja wa Kisovyeti kwa lugha ya Kirusi.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kirusi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.