Taiga
Taiga (kwa Kiingereza[1] pia boreal forest [2] au snow forest [3]) ni jina la maeneo makubwa ya misitu kaskazini mwa dunia inayofanywa na aina mbalimbali ya miti ya misunobari, katika Eurasia pia pamoja na mibetula. Takriban 29% za misitu yote duniani ni aina ya taiga.
Taiga inafunika sehemu kubwa za Alaska, Kanada, Uswidi, Ufini, Norwei, Kazakhstan ya kaskazini na Urusi (hasa Siberia) pamoja sehemu nyingine za kaskazini za Marekani.
Maeneo ya taiga yako upande wa kusini wa kanda la tundra. Katika Urusi taiga inafuatwa na kanda la mbuga baridi kusini mwake.
Kwa jumla tabianchi kwenye taiga ni baridi sana kwa miezi mingi ya mwaka[4]. Majirajoto ni fupi, kwa kawaida miezi 1-2 pekee. Taiga ya Siberia wastani ya halijoto wakati wa baridi ni kati ya -6°C na -50°C.[5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Asili ya jina iko katika lugha za Kiturki
- ↑ msitu wa kaskazini
- ↑ msitu wa theluji
- ↑ "radford:Taiga climate". Radford.edu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-09. Iliwekwa mnamo 2011-02-21.
- ↑ Encyclopedia Universalis édition 1976 VOL.2 ASIE – Géographie physique, page 568 (Kifaransa)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Boreal Forests/Taiga (WWF)
- Terraformers Canadian Taiga Conservation Foundation Ilihifadhiwa 28 Februari 2011 kwenye Wayback Machine.
- Arctic and Taiga (Canadian Geographic) Ilihifadhiwa 12 Julai 2006 kwenye Wayback Machine.
- Coniferous Forest. Earth Observatory. NASA. [1] Ilihifadhiwa 4 Julai 2008 kwenye Wayback Machine..
- Taiga Rescue Network (TRN) Ilihifadhiwa 6 Aprili 2013 kwenye Wayback Machine. A network of NGOs, indigenous peoples or individuals that works to protect the boreal forests.
- Index of Boreal Forests/Taiga ecoregions at bioimages.vanderbilt.edu Ilihifadhiwa 5 Septemba 2012 kwenye Wayback Machine.
- The Nature Conservancy and its partners work to protect the Canadian Boreal Forest Ilihifadhiwa 13 Desemba 2010 kwenye Wayback Machine.
- Slater museum of natural history: Taiga Ilihifadhiwa 16 Machi 2009 kwenye Wayback Machine.