Nenda kwa yaliyomo

Watetezi wa imani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Yustino katika picha takatifu ya Urusi.

Watetezi wa imani ni jina walilopewa baadhi ya mababu wa Kanisa waliojitokeza kutetea Ukristo dhidi ya hoja za Wayahudi na Wapagani, tena dhidi ya dhuluma ya Dola la Roma dhidi ya Wakristo.

Pengine kwa utetezi wa namna hiyo katika Kiswahili linatumika neno "Apologetiki" kama katika lugha nyingi kwa kutohoa neno la Kigiriki ἀπολογία, apologia, "utetezi wa sauti, hotuba ya utetezi"[1].

Utetezi wa Ukristo ulihitajika mapema, hivyo unajitokeza katika Agano Jipya lenyewe, kwa mfano katika nyaraka za Mtume Paulo.

Baadaye uliendelezwa katika maandishi ya waumini kama vile Yustino mfiadini, Irenei, Tertullianus, Origen na Agostino wa Hippo.

Dhuluma ya kwanza yalitokea mwaka 64 BK, ya mwisho mwaka 309 BK. Katika kipindi hicho kirefu, vilirudia tena na tena vipindi vya mateso vikifuatana na vipindi vya amani. Lakini miaka yote Ukristo ulikuwa dini isiyo halali. Kila mara mateso yaliweza kuanza upya.

Basi, wasomi hao na wengineo walijitokeza kuandika vitabu ili kutetea Ukristo dhidi ya masingizio na chuki ya wengi; walifafanua imani ilivyo na kuonyesha kwamba maisha ya wafuasi wa Yesu hayaendi kinyume cha sheria za dola, hivyo dhuluma dhidi yao hazikubaliki.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "ἀπολογία". Blue Letter Bible-Lexicon. Iliwekwa mnamo 7 Mei 2012. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |unused_data= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Watetezi wa imani kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.